Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Isere Sports ya jijini Dar es Salaam imepewa rasmi jukumu la kuuza vifaa vyote vya Klabu ya Simba vyenye nembo halali.
Mwenyekiti wa Wadhamini wa Klabu ya Simba, Hamisi Kilomoni akizungumza na waandishi wa habari alisema kuanzia sasa wakala atakayeuza bidhaa za Simba ni Isere Sports.
Alisema msako mkali wa kukamata jezi, kaptula,bendera,riboni ambapo kampuni iliyopewa jukumu la kukamata mali zote za Simba, Tume ya Ushindani ambapo jumla ya vifaa mbalimbali vilivyokamatwa hadi sasa vina thamani ya sh. mil.44.2.
Alisema Simba inatoa muda hadi kufikia Jumatatu ijayo bidhaa zote zisalimishwe klabuni vinginevyo msako ukiwabaini wahusika wasiilamu klabu hiyo.
Mkurugenzi wa Masoko wa Isere Sports, Abbas Isere alisema kazi aliyokabidhiwa itafanikiwa kama wanachama na mashabiki wa klabu hiyo watashiriki kupiga vita bidhaa bandia zinazoingizwa nchini kutumia nembo ya Simba.
Msemaji wa Simba, Ezekiel Kimwaga alisema msako huo wa bidhaa bandia za Simba ni endelevu na watakaokamatwa wanatumia nembo za klabu hiyo kujitajirisha wanafikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Mpaka sasa mali bandia za Simba zilizokamatwa ni jezi 1,261,kaptura za Simba 31,Ribbon za Simba 228,bendera za Simba 189, na urembo wa kuvaa mkononi 1,248.
mwisho
No comments:
Post a Comment