TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION
TANGAZO SHIWATA
Monday, 12 August 2013
Mkuutano wa Uwaka Dekania ya Ukonga kufanyika Segerea Jumapili
Na Mwandishi Wetu
VIONGOZI watano wa Utume wa wanaume Wakatoliki (UWAKA) wa Dekania ya Ukonga wanafanya mkutano wa kwanza kutoka uongozi mpya uchaguliwe utakaofanyika Jumapili katika Parokia ya Roho Mtakatifu Segerea.
Katibu wa UWAKA Dekania ya Ukonga, Bw. Peter Mwenda katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana alisema mkutano huo ni kwa ajili ya kutambulisha uongozi mpya na kuweka mikakati ya kutafuta fedha a ukarabati wa Kituo cha Hija cha Pugu na jukumu la kulea wadada wadogo, Mbagala.
Dekania ya Ukonga inaundwa na Parokia 16 ambazo ni Kinyerezi, Buza, Yombo Dovya, Kisarawe, Kitunda, Mongo la Ndege, Vituka, Chanika, Ukonga, Pugu, Vingunguti,Kipawa, Tabata,Segerea,Mji Mpya Relini na Kiwalani.
Wakati huo huo Viongozi wawili wa Dekania ya Ukonga wamechaguliwa kuongoza UWAKA Jimbo Kuu la Dar es Salaam katika uchaguzi uliofanyika Parokia ya Mtakatifu Joseph Jumapili.
Katibu wa UWAKA Parokia ya Ukonga, Bw. Dismas Kachem amechaguliwa tena kuendelea na wadhifa wa Mwenyekiti na Katibu wa chama hicho wa Parokia ya Pugu, Bw. Valentine Mhagama amechaguliwa kuwa Katibu Msaidizi wa Jimbo.
Makamu Mwenyekiti alichaguliwa kuwa Bw. Amadeus Mosha kutoka Parokia ya Mavurunza, Katibu alichaguliwa kuwa Julius Kasonso kutoka Parokia ya Kurasini na Mweka Hazina alichaguliwa kuwa Richard Rweyemamu kutoka Parokia ya Tegeta.
mwisho
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment