Amigolas katikati akiimba Enzi zake akiwa na bendi yake ya zamani
Twanga Pepeta wakwanza kulia ni Kiongozi wa bendi hiyo Luiza Mbutu na
kushoto ni Greyson Semsekwa wakiwa katika moja ya onesho.
BAADA ya kudumu katika bendi ya The
African Stars ‘Twanga
Pepeta’ Hamis Kayumbu ‘Amigolas’ ambaye pia ni kati ya wasanii waasisi
wa bendi hiyo sasa amevunja ukimya na kukiri kuwa ameamua kugeukia
muziki wa Hotelini ambao anaona utamlipa kwa sasa.
Amigolas mwenyewe amethibitisha hilo kwa kuzungumza na
mwandishi wa habari hii kwamba ni kweli ameamua kuipa kisogo bendi yake ya
zamani ‘Twanga Pepeta’ na kwamba hivi sasa yeye na bendi yake hajaitaja jina
kuwa wanajipanga kuanza mazoezi na baadaye watazungumza na vyombo mbalimbali vya habari katika mkutano maalumu.
“Nikweli nimeanzisha bendi ambayo itakuwa ikipiga muziki
katika hoteli mbalimbali pia tutakuwa tunaporomosha muziki kwenye kumbi
mbalimbali ,lakini kwa sasa ni mapema sana kusema hilo hivyo tunajipanga kwani
tunatarajia pia kwenda nje ya nchi kupiga muziki” alisema Amigolas.Aidha aliongeza kwa kusema kuwa hadi leo, jana alikuwa bado hajawaaga
viongozi wa ASET lakinianaweka mambo
yake sawa na atapanga kwenda kuaga rasmi.
Wakati akitimka kimyakimya itakumbukwa , Mwaka 2008 Amigolas alipanga kung’atuka
katika bendi hiyo lakini akabaki , kadhalika mwaka jana alitangazwa na vyombo
vya habari kuhama bendi hiyo huku uthibitisho wa kutosha kutoka kwake
ukikosekana tofauti na mwaka huu ammbapo amekiri.
Mbali ya Amigo wasanii wengine wanaounda bendi hiyo ni pamoja na Mpapasa
Kinanda mahiri Victor Mkambi na Rapa machachari Diouf.
Akizungumzia hilo Mkurugeni wa Kampuni ya
ASET , Asha Baraka alisema kwamba wanaahidi kumpa sapoti kubwa Amigolas, “Tutampa
sapoti ya kutosha Amigo na tunamtakia kila la kheri aendako kwani muziki wa
sasa ni mchakamchaka nay eye kutokana na umri pamoja na afya yake kwa sasa
hawezi mbiombio zilizopo kama jinsi alivyokuwa zamani”.
Anaongeza kwa kusema kuwa zamani Amigo aliweza kufanya shoo
kuanzia Jumatano, Alhamisi, Ijumaa, Jumamosi, Jumapili lakini kwa muda wa miaka
miwili sasa hata katika bendi amekuwa akifanya shoo moja tu hivyo hadi hapo
utaona kwamba alishabadilika na kwa staili aliyoichagua ya kuhamia katika
muziki wa hotelini ataweza kwani ule hauna makeke sana” alisema Asha.
No comments:
Post a Comment