TANZANIA BOXING NEWS: UCHAGUZI BFT JULAI 7
Uchaguzi wa viongozi wa BFT uliopangwa Kufanyika tarehe 7/7/2013 jijini Mwanza, utafanyika kwa tarehe hiyo kama ulivyopangwa.
Kikao
cha kamati ya utendaji ya BFT kilichofanyika juzi katika ofisi za BFT
kikiongozwa na Rais wa shirikisho Joan Minja kimesisitiza kuwa uchaguzi
utafanyika kama ulivyopangwa na haujaairishwa kama baadhi ya kikundi
cha watu wachache wanaojiita wadau wanavyoweka pingamizi na kupotosha
kwa kuwashawishi wajumbe wa mkutanao mkuu hasa kutoka mikoani
kutohudhuria mkutano huo wa uchaguzi,kwa manufaa yao binafsi na
kinyume na katiba yetu.
Upotoshaji
huo unafanywa na Akaroly Godfrey aliyekuwa kiongozi katika uongozi
uliojiudhuru kutokana na kashfa za kusafirisha madawa ya kulevya
na kusababisha Tanzania kufutwa uanachama na chama cha ngumi cha
dunia (AIBA) na kusababisha kutoshiriki mashindano,mikutano na
shughuri zote za kimataifa za chama cha ngumi cha Dunia AIBA. Naomba
wadau na serikali kuwa makini na watu wanaoshawishi kwa lengo la
masilahi yao binafsi na kusababisha michezo kudolola badala ya kusonga
mbele.
Fomu
za uchaguzi zilishaanza kutolewa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT)
toka tarehe 4//2013 na zitaendelea kutolewa hadi tarehe 4/7/2013 jijini
Mwanza na tarehe hiyo ndio itakuwa siku ya mwisho ya kuchukua na
kurudisha
fomu, tarehe 5/7/2013 itatakuwa siku ya usaili na utafanyika jijini
mwanza, tarehe 6/7/2013 kupitia pingamizi na kuzitolea maamuzi na tarehe
7/7/2013 ndio siku ya uchaguzi.
Kimsingi taratibu zote za kuitisha uchaguzi kwa mujibu wa katiba yetu zimezingatiwa na zimekamilika.
Aidha BFT inatoa tamko kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu kufika katika
uchaguzi uchaguzi, ili kupata viongozi halali kwa mujibu wa katiba,
waendelee na shughuri za kuendeleza mchezo wa ndondi na kuaandaa timu
ya taifa kushiriki katika mashindano ya Afrika nchini Mauritius Sept. 2013
BFT
inatoa wito kwa watu wote wenye sifa, nia, moyo na uwezo wa kuongoza
wajitokeze kuchukua fomu za kugombea uongozi kwani wakati ndio huu.
No comments:
Post a Comment