Tuesday, January 8, 2013
FIFA YATANGAZA MAJINA YA WAAMUZI WA TANZANIA WATAKAOVAA BEJI ZAKE KWA MWAKA 2013
WANAUME:
IBADA Ramadhan Kibo
MBAGA Oden Charles
MUJUNI Israel
WAZIRI Waziri Sheha
Assistant Referee
BULALI Josephat Deu
CHACHA Ferdinand
CHANGWALU Hamis Ramadhani
KANYENYE John Longino
KINDULI Alli
KLEMENCE ERASMO Jesse
MPENZU Samuel Hudson
WANAWAKE:
GAMBA Judith Andrew
Assistant Referee
MAKAME Mwanahija Foum
CAF YAIPIGA JEKI TFF
SHIRIKISHO la soka barani Afrika (CAF) limetoa ufadhili kwa
Shirikisho la soka Tanzania (TFF) katika kurabati kituo chake cha michezo
kilichopo Karume jijini Dar es Salaam.
Ufadhili huo ni sehemu ya mpango wa kusaidia wanachama
wake katika dhima nzima ya kuchangia maendeleo ya soka ambapo utahusisha kukarabati maeneo mbalimbali ya mpango huo ikiwemo uwanja
na hosteli zilizopo Karume.
Tayari zimeshatangaza tenda kwa makampuni
mbalimbali ili kujitokeza kwa ajili ya kuendesha mradi huo kabla ya bodi husika
kukaa na kuteua kampuni itakayofanya ukarabati huo.
TCCA FAMILY DAY ILIVYOFANA
watoto wa wafanyakazi wa mamlaka ya usafiri wa anga Tanzania TCCA, walioshiriki katika Famillya Day wakishindana kukimbia namagunia.
Wafanyakazi wa tcaa wakicheza mpira wa mikono vollybo wakati wa familly day iliyofanyika jijini Dar es Salaam,
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usfiri wa Anga Tanzania (TCAA) Wakishindana kuvuta kamba wakati wa sherehe za familly day iliyofanyika jijini dar es salaam.
Wafanyakazi wa tcaa wakicheza mpira wa mikono vollybo wakati wa familly day iliyofanyika jijini Dar es Salaam,
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usfiri wa Anga Tanzania (TCAA) Wakishindana kuvuta kamba wakati wa sherehe za familly day iliyofanyika jijini dar es salaam.
watoto wakishindana kukukmbia na vijiko huku wameweka mayai
MIRAJI KIKWETE ATEULIWA KUWA MAKAMU WA RAIS IBF AFRIKA
Shirikisho
la Ngumi la Kimataifa Africa (IBF/Africa) limemteua bwana Miraji Mrisho
Kikwete kuwa Makamu wa Rais anayeshughulikia maendeleo ya vijana katika
bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati. Uteuzi wa Miraji
unaanza January mwaka mpya2013.
Katika
kumteua Miraji, Rais wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na
Mashariki ya Kati bwana Onesmo Ngowi alisema kuwa Miraji ana uwezo wa
kuwahamasisha na kuwaunganisha vijana katika shughuli za maendeleo.
Aliendelea
kusema kuwa Miraji atakuwa anawahamashisha vijana, kuwaunganisha,
kuwajengea uwezo wa kimaendeleo yatakayoratibiwa na IBF.
Aidha,
Rais huyo alisema kuwa Miraji atakuwa anabuni njia mbalimbali za
kuwaunganisha vijana wa Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati ili
waweze kufaidika na miradi ya IBF ambayo inalenga kwenye elimu, kujenga
vipaji pamoja na kuwaunganisha kwenye biashara ya utalii wa michezo.
Katika
mkutano wake wa mwaka uliofanyika katika jiji la Honolulu, jimbo la
Hawaii, nchini Marekani hivi karibuni IBF iliupokea mradi wa “Utalii wa
Michezo” uliobuniwa na kuwakilisshwa na Rais wa IBF katika bara la
Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati Mtazania Onesmo Ngowi.
Lengo
kuu la mradi huu ni kulifanya bara la Afrika hususan Tanzania kuwa
kitovu kikuu cha “Utalii Michezo” hivyo kujenga uchumi imara. Nchi za
Tanzania na Ghana ziliteuliwa kuwa nchi za mfano kwenye mradi huu.
Katika
mradi huu, IBF itatumia mtandao walionao katika nchi zaidi ya 203
duniani kuhamasisha wanachama wake na famlia zao, wapenzi pamoja na
marafiki zao kuja Afrika/Tanzania kutalii pamoja na kuwekeza katika
miradi mbalimbali.
Uteuzi
wa Miraji utasaidia kuwaunganisha vijana ili waweze kuchangia na
kufaidika na biashara ya utalii kwenye mradi huu umefanywa wakati
muafaka.
Miraji
ambaye ni Mjasiliamali amejipambanua katika maendeleo ya jamii na ana
mchango mkubwa sana katima kuendeleza vijana nchini Tanzania.
Rais
Ngowi alimwelezea Miraji kama tegemeo ambalo vijana wanalihitaji kwani
wanahitaji uhamasishaji wa hali ya juu na Miraji ana uwezo wa kufanya
kazi hiyo kwa ufanisi mkubwa kwani alishawahi kuifanya kwa kipindi
kitefu.
Miraji
Mrisho Kikwete ni msomi wa chuo kikuu cha nchini Oman ambako amesomea
elimu ya utawala wa biashara ambayo ndiyo lengo kuu la uteuzi wake. Ana
haiba ya kupendwa na vijana pamoja na uwezo wa kujichanganya nao.
SIMBA, AZAM FC KUKWAANA NUSU FAINALI MAPINDUZI CUP
MABINGWA
wa ligi kuu bara Simba Sc watakutana na Mabingwa wa kombe la mapinduzi
Azam fc katika nusu fainali ya micchuano ya kombe la Mapinduzi
itakayopigwa keshokutwa, katika uwanja wa Aman Visiwani zanzibar.
MESSI ATWAA TUZO YA BALLON d' OR
Mshambulizi wa Barcelona na timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi ameshinda tuzo ya Ballon d'Or kwa mwaka wa nne mfululizo.
Messi,
25, alifunga jumla ya magoli 91 mwaka wa 2012 na aliwashinda wachezaji
wengine Andres Iniesta wa Barcelona na Christiano Ronaldo wa Real
Madrid.
Licha
ya kufunga idadi hiyo ya magoli, timu yake ya Barcelona haikunyakuwa
kombe la ligi kuu ya Uhispania ay kombe la klabu bingwa barani Ulaya
mwaka uliopita.
Abby Wambach, alishinda tuzo kwa upande wa kina dada naye Vicente del Bosque, akituzwa kuwa kocha bora.
Timu bora ya kwana ilijumuisha wachezaji wanaoshiriki katika ligi ya Uhispania pekee.
Messi
alitangazwa mshindi wa tuzo hiyo ya the Ballon d'Or, tuzo ambayo
hukabithiwa mchezaji bora wa mwaka katika sherehe iliyofanyika mjini
Zurich
Messi
alikuwa miongoni mwa wachezaji watatu walioteuliwa na jopo la wandishi
wa habari na makocha wa timu za taifa, manaodha wa timu hiyo wakiwa ni
pamoja na Iniesta na Ronaldo.
Mesi
sasa ni mchezaji wa kwanza kuwahi kushinda tuzo hiyo ya Ballons d'Or,
kwa miaka minne mfululizo, rekodi anayoshikilia na aliyekuwa mchezaji wa
Ufaransa na rais wa UEFA kwa sasa Michel Platini.
Kikosi cha wachezaji bora wa mwaka 2012
•Iker Casillas (Real Madrid)
•Dani Alves (Barcelona)
•Gerard Pique (Barcelona)
•Sergio Ramos (Real Madrid)
•Marcelo (Real Madrid)
•Andres Iniesta (Barcelona)
•Xabi Alonso (Real Madrid)
•Xavi (Barcelona)
•Cristiano Ronaldo (Real Madrid)
•Radamel Falcao (Atletico Madrid)
•Lionel Messi (Barcelona)
•Dani Alves (Barcelona)
•Gerard Pique (Barcelona)
•Sergio Ramos (Real Madrid)
•Marcelo (Real Madrid)
•Andres Iniesta (Barcelona)
•Xabi Alonso (Real Madrid)
•Xavi (Barcelona)
•Cristiano Ronaldo (Real Madrid)
•Radamel Falcao (Atletico Madrid)
•Lionel Messi (Barcelona)
CHANZO:BBC SPORTS
No comments:
Post a Comment