SAFARI YA SIMBA OMAN YANUKIA, TAYARI PASIPOTI ZA WACHEZAJI ZATUMWA
UONGOZI
wa klabu ya Simba umepeleka hati za kusafiria za wachezaji wake nchini
Oman ili kuweza kupatiwa vibali vitakavyowaruhusu kuingia nchini humo.
Simba
ambayo kwa sasa ipo Visiwani Zanzibar ikishiriki michuano ya kombe la
Mapinduzi, awali ilipanga kwenda Oman kesho kwa ajili ya kambi maalum ya
kujiandaa na ligi kuu ya Vodacom na michuano ya kimataifa.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi jana, Mwenyekiti wa Simba Alhaj Ismail Aden
Rage alisema jana kwamba wamelazimika kuzitumna hati hizo Oman kutokana
na utaratibu wa sasa unavyohitajika.
“Viza
zote za kuingia nchini Oman kwa sasa zinatakiwa kuomba hukohuko kwao
hivyo tumemetuma hati za kusafiria za wachezaji na viongozi
watakaokwenda na baada ya hapo tutapanga safari,”alisema
Alisema
mara baada ya kupatiwa viza ndipo wataamua rasmi ni lini watakwenda
huko lakini wanatarajia safari yao itakuwa kuanzia Januari 10 mwaka
huu,huku pia wakiangalia mwenendo wa timu yao katika kombe la Mapinduzi.
Rage
aliongeza kuwa iwapo watafanikiwa kwenda Oman, pamoja na mazoezi ya
kawaida pia watacheza michezo kadhaa ya kujipima nguvu na timu za huko
ikiwemo Fanja Fc.
Mabingwa
hao watetezi wa ligi kuu ya Vodacom walimaliza mzunguko wa kwanza na
kushika nafasi ya tatu nyuma ya Azam Fc na Yanga iliyoshika nafasi ya
kwanza, hivyo uongozi uliamua kuipeleka nje ya nchi kwa ajili ya kuweka
kambi.
Aidha,
mabingwa hao wataanza kampeni yao katika klabu bingwa Afrika kwa
kucheza na Recreativo de Libolo ya Angola kati ya Februari 17 na 19 kwa
kucheza nyumbani.
No comments:
Post a Comment