Lulu aachiwa kwa dhamana
.Amwaga chozi la furaha
Na Mwandishi Wetu,Mahakama Kuu
MSANII wa Filamu Elizabert Michael 'Lulu' amwaga chozi katika viwanja vya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam baada ya kutimiza masharti matano ya dhamana na kuruhusiwa kurudi uraiani.
Lulu alimwaga chozi hilo pamoja na ndugu zake alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari na kutoa shukurani zake kwa mwenyezimungu na watu wote waliomsaidia katika kesi yake.
Kwa maana hiyo pindi kesi yake ya msingi itakapopangiwa Jaji na kuanza kusikilizwa,Lulu atakuwa akitokea nyumbani kwenda mahakamani tofauti na awali alipokuwa akitokea Mahabusu ya Segerea.
"Nawashukuru watu wote,na nilikuwa naomba watu waendelee kuniombea,kwa ajili hii ni dhamana tu lakini kesi bado, nina na safari ni ndefu,nashukuru wale wote waliokuwa na mimi kwa hali yoyote na zaidi namshukuru Mungu kwani yeye ndiyo kila kitu" alisema huku akimwaga machozi.
Lulu alifanikiwa kutimiza masharti ya dhamana saa 9:55 jioni na kuondoka katika viwanja vya mahakama hiyo kwa gari namba T 480 CFX Toyota Land Cruiser.
Awali Lulu alifika katika viwanja vya mahakama hiyo saa 7:50 mchana akitokea katika mahabusu ya Segerea baada ya kupelekewa hati ya kuitwa mahakamani.
Mshtakiwa huyo aliletwa mahakamani hapo na gari la Magereza STK
2823 Landrover huku akisindikizwa na askari watatu wa kike wa Magereza na mmoja wa kiume.
Masharti ya dhamana ya Lulu yalithibitishwa na Naibu Msajili wa mahakama hiyo Francies Kabwe ambaye alipitia masharti yote na kuona kama yametimizwa.
Akiwa mahakamani hapo Lulu alidhaminiwa na wadhamini wawili ambao ni Frorian Mmtafugwa mfanyakazi kutoka Wizara ya Ardhi na Verus Kataruga kutoka Wizara ya Afya.
Kwa upoande wake wakili Fulgency Masawe anayemtetea Msanii huyo alisema pamoja ya kupata dhamana bado kesi yake ya msingi inaendelea na bado haijapangiwa jaji wala tarehe ya kuanza kusikilizwa.
Naye Wakili Peter Kibatala alisema kuwa kwa sasa Lulu anaenda nyumbani kwao kwa wazazi wake na wanategemea kupata ushirikiano mkubwa kutoa kwake.
Katika hatua nyingine Kibatala aliishukuru Mahakama hiyo kwa kuelewa dhamana ni haki ya mshtakiwa pamoja na msajiri kwa kushughulikia dhamana hiyo hadi mwisho.
Januari 28 mwaka huu Jaji Zainabu Mruke wa Mahakama hiyo alisikiliza maombi ya dhamana ya Msanii huyo na kuyaridhia na kutoa dhamana.
Jaji Mruke alitoa dhamana kwa mshtakiwa huyo kwa kutoa masharti matano ambayo ameyatimiza jana na kuthibitishwa na msajiri wa mahakama hiyo.
Masharti hayo ni kuwasilisha kwa msajiri wa mahakama hiyo hati zake zote za kusafiria.
Sharti lingine ni kutosafiri nje ya Jiji la Dar es Salaam bila idhini ya msajili huyo, kujiwakilisha (kuripoti) kwake kila tarehe mosi ya kila mwezi hadi kesi yake itakapokwisha.jingine ni kwamba kuwa na wadhamini wawili ambao ni wafanyakazi wa serikalini watakaosaini hati ya dhamana ya sh.milioni 20 kila mmoja.
Katika kesi hiyo ,Lulu anakabiliwa na kesi ya kuua bila kukusudia Na. 125/2012 msainii mwenzake marehemu Steven Kanumba.
Msanii huyo amepata dhamana hiyo wakati kesi yake ya msingi ya kuua bila kukusudia bado haijapangiwa tarehe ya kuanza kusikilizwa wala jaji.
MWISHO
No comments:
Post a Comment