TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Tuesday, 8 May 2012

VICOBA Ukonga kuanzisha SACCOS

Na Peter Mwenda

WANAWAKE wanachama wa Benki ya Jamii (VICOBA) Jimbo la Ukonga wameshauriwa kuanzisha Benki ya Kukopa na Kuweka (SACCOS) ili kuinua mitaji ya biashara zao.

Hayo yalisemwa jana na Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Bi. Eugen Mwaiposa wakati akizindua vikundi 15 vya VICOBA katika Kata mbili za Kitunda na Kivule, Ilala Dar es Salaam.

Alisema akinamama hao wakianzisha SACCOS yao wataongeza kiwango chao kukopa fedha ambazo zinaongeza mitaji ya biashara zao.

"Mkianzisha SACCOS ya VICOBA katika Jimbo la Ukonga nitawaombea fedha za Mfuko wa Jimbo ili ziwasaidie kuimarisha mitaji yenu, akinamama wote wa Jimbo la Ukonga mtanufaika" alisema Bibi Mwaiposa.

Mbunge Mwaiposa alisema Serikali na jamii kwa ujumla inawategemea wanawake kwani ndiyo wasimamizi wa fimilia hivyo ni wakati kwao kujiendeleza na kuongeza elimu ya kuendesha biashara zao.

Bi. Mwaiposa alitoa wito kwa wanaume kuanzisha VICOBA ili kujikwamua na umasikini na kusaidia kusomesha watoto kwa kuwalipia karo na kuanzisha biashara kusaidia na wake zao.

Katika risala ya vikundi 10 vya Vicoba iliyosomwa na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mzinga, Kitunda Bi. Flora Lemu ilisema kuwa wamekuwa wakishirikiana kukopeshana fedha kwa ajili ya kusomesha watoto, kusaidiana katika maafa.

Bi. Lemu alisema vikundi hivyo vinavyo mtaji wa sh. mil. 90 ambazo zinakopeshwa kwa wanachama kufuikia sh. 500,000 kwa mwanachama.

Alisema vikundi hivyo ninavyo wanachama 450 na wengine wanaendelea kuunda vikundi vingine kwa ajili kukabiliana na umasikini.

Mwenyekiti wa vikundi hivyo Bi. Advela Ruge alisema wanahawasisha akinamama wengine kuanzisha vikundi vya VICOB ili kila mwanamke ashiriki katika kuongeza uchumi wa familia zao.

mwisho

No comments:

Post a Comment