Haruna
Moshi akionyesha makeke yake langoni mwa timu ya Malawi katika mchezo
wa kirafiki uliochezwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam..
Mshambuliaji
wa Timu ya Taifa Stars,Haruna Moshi "Boban" akiwachachafya mabeki wa
timu ya Malawi katika mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye uwanja wa
Taifa jijini Dar es Salaam.
Hatari langoni mwa timu ya Malawi.........
Mchambuliaji
wa Timu ya Taifa,Mbwana Samatta akijaribu kumtoka Beki wa Timu ya
Malawi,Limbikani Mzava katika mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye
uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Kipindi cha cha mchezo huu
kimemalizika huku timu zote mbili zikitoka bila kufungana.
Wachezaji wa Timu ya Taifa wakitoka uwanja baada ya kumalizika kwa Mchezo huo.
Taifa
Stars wala Malawi hakuna aliefanikiwa kupata goli, hata hivyo wamalawi
wameshambulia mara nyingi katika lango la Taifa Stars katika kipindi cha
kwanza, lakini uimara wa mabeki pamoja na Golikipa Juma Kaseja
umesaidia sana Taifa stars kutofungwa , Taifa Stars yenyewe imefanya
mashambulizi ya hatari,hata hivyo haikuwa bahati yao ambapo mpaka mwisho
wa mchezo huo timu hizo zimetoka sare ya 0-0.
Timu ya Malawi iko safarini kuelekea nchini Uganda ambako itacheza na timu ya Uganda Cranes.





No comments:
Post a Comment