TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Monday, 21 May 2012

MBUNGE WA CCM AZUIWA KUMUONA LULU SEGERA


ALIYEKUWA Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Frederick Mwakalebela amesikitishwa na kitendo cha kuzuiwa kwenda kumjulia hali, mahabusu Elizabeth Michael aliyewekwa katika gereza la Segera, Dar es Salaam.
Akizungumza na BIN ZUBEIRYhttp://bongostaz.blogspot.com/, Mwakalebela (pichani kushoto) ambaye pia aliwahi kugombea ubunge wa Iringa mjini kwa tiketi ya CCM na kukwama katika hatua za awali, alisema kwamba alijihimu yeye na familia yake kwenda kumuona Lulu anayeshikiliwa kwa tuhuma za mauaji ya mwigizaji mwenzake, Steven Kanumba, lakini akazuiwa.
"Walinizuia wakisema hadi wapewe ruhusa kutoka ngazi za juu, nilifanya jitihada za kupata kibali, lakini sikufanikiwa, imenisikitisha sana,"alisema Mwakalebela, ambaye alimtumia Lulu katika filamu yake ya Septemba 11, iliyoshirikisha mastaa wengine kadhaa wa soka, akiwemo Juma Kaseja, kipa namba moja wa taifa.
Mwakalebela alisema pamoja na Lulu kucheza Septemba 11,pia nimtu wa karibu wa familia yao.

No comments:

Post a Comment