Gwiji
la Muziki wa Taarabu nchini, na Mshindi wa Tuzo ya Mtumbuizaji bora wa
Kike, Hadija Kopa akifanya makamuzi katika tamasha maalum la Washindi
wa Kili Music Award 2012 kwenye uwanja wa Ushirika Moshi Mkoani
Kilimanjaro jana.
Msanii
AT kutoka Zanzibar akitumbuiza jukwaani na wacheza sho wake wakati wa
show maalum ya Washindi wa Kili Music Award kwenye uwanja wa Ushirika
Moshi Mkoani Kilimanjaro jana.
Barnaba
Boy ambaye ni mshindi wa Tuzo ya Mwimbaji Bora wa Kiume akimbo jukwaani
hii leo wakati wa show maalum ya Washindi wa Kili Music Award kwenye
uwanja wa Ushirika Moshi Mkoani Kilimanjaro jana.
Mkali
wa Bongo fleva Ali Kiba akiimba jukwaani hii leo wakati wa show maalum
ya Washindi wa Kili Music Award iliyofanyika kwenye uwanja wa Ushirika
Moshi Mkoani Kilimanjaro jana.
Msanii
anae kuja juu Omy Dimpoz nae akikamua jukwaani wakati wa show maalum ya
Washindi wa Kili Music Award mkoani Mwanza katika Uwanja wa Kirumba
leo.
Mkali wa HIP HOP Roma kiwakilisha vilivyo katika jukwaa.
Suma
Lee nae alishambulia jukwaa vilivyo na kuleta raha kwa mashabiki katika
wakati wa show maalum ya Washindi wa Kili Music Award kwenye uwanja wa
Ushirika Moshi Mkoani Kilimanjaro jana.
Huu ni umati ulifurika
Na Mwandishi Wetu
GWIJI
la Taarab nchini Tanzania kutoka kundi la TOT, Hadija Omary Kopa na
wasanii wa muziki wa Bongo fleva, Ali Kiba, Omy Dimpoz, Roma Mkatoliki
AT, pamoja na wakali wa Ragge Warriors walikonga vilivyo nyoyo za
mashabiki wa burudani mjini Moshi na kudhihirisha uhalali wao wa kutwaa
Tuzo mbalimbali za Kili Music 2012.
Wasanii
hao waliokuwa wakitumbuiza katika Tamasha maalum la Kili Music Award
Winners Tour lililofanyika jana kwenye Uwanja wa Ushirika mjini hapa.
Licha
ya hali ya hewa kuwa ya mvua na manyunyu ya hapa na pale wakati wote wa
tamasha hilo lakini wakazi wa mji wa Moshi na vitongoji vyake jana
walivunja rekodi ya Tamasha hilo kwa kujitokeza kwa wingi uwanjani hapo
tofauti na mikoa mingine ya Dodoma na Mwanza ambako tayari Tanasha kama
hilo limefanyika.
Kabla
ya washindi wa Tuzo za Mziki za Kilimanjaro 2012 kupanda jukwaani
walianza kupandaa chipoukuzi wa tatu wealio chuana vikali na mashabiki
kumpitisha Msanii Sungura aliyeonekana kupagawisha vilivyo kwa wimbo
wake wa Ndizi yangu.
Walianza
jukwaani kupanda washindi wa Tuzo Bora ya Wimbo wa Ragge ambayo
ilitwaliwa na kundi la Warriors from East waiotamba na vibao vyao kadhaa
na kupiga jukwaani zaidi ya saa moja na kibao cha Arusha Gold
kilichopawa tuzo kikiburudisha vilivyo na live show yao.
Mkongwe
wa Taarab, Hadija Omary Kopa aliiudhihirishia umma wa wana Kilimanjaro
kuwa yeye ni Mtumbuizaji bora wa Kike baada ya kupanda jukwaani na
kuimba nyimbo zake kadhaa zilizojaa vijembe na mashairi ya ukweli ya
taarab kutoka kundi lake la TOT huku uchezaji wake ukishangilia mwanzo
hadi mwisho kwa jinsi alivyokuwa akiutikisa mwili wake.
Mkali
kutoka Zanzibar ambaye ni mshindi wa Tuzo Wimbo Bora wenye Vionjo vya
Kiasili AT nae alipanda jukwaani nyuma ya Hadija Kopa na kutoa burudani
ya nguvu na wimbo wa Vifuu Utundu amabao ulimpa tuzo aliucheza vilivyo
na wanenguaji wake waili wa kike.
Akitanguliwa
jukwaani na wacheza show wake machachari alikuwa ni mshindi wa Tuzo
mbili za Kili Music Award 2012, Suma Lee aliyenyakua tuzo za wimbo bora
wa Afro Pop kupiria kibao chake cha Hakunaga na Wimbo bora wa mwaka
ambao pia ni hakunaga alikamua sawasawa.
Jukwaa
lilishikwa na Omy Dimpoz kwa kuimba nyimbo zake kadhaa ikiwapo ile
iliyo mpa tuzo ya Wimbo bora wa Kushirikishwa ya Nai Nai ambapo stejini
pia alipanda Ali Kiba na kumsindikiza live katika kibao hicho na kufumua
yowe na shangwe kutoka kwa mashabiki.
Ali
Kiba alibaki jukwaani hapo na vijana wake kumfuata kutoa shukrani zao
za kupata kura zilizo wapa ushindi wa tuzo ya Wimbo bora wa Zouk Rhumba
kupitia wimbo wa Dushelele. Kiba alilimudu jukwaa vyema kwa kucheza
sambamba na vijana wake mwanzo mwisho.
Jukwaa
lilichuliwa kwa muda na Mshindi wa Tuzo ya Mwimbaji bora wa Kiume,
Barnaba na kuwashukuru ndugu zake wa Moshi kwa kumpa kura na kuwa Mchaga
anaeimba vyema.
Pazia
la Wasanii washindi wa tuzo za Kili Music Award 2012 wanaofabnya ziara
na waliobahatika kufika mjini Mosho mkoani Kilimanjaro lilifungwa na
Roma Mkatoliki a.k.a Mpare wa milimani aliyeshambulia jukwaa kwa nyimbo
zake kadhaa za mistaari ya maandiko.
Roma
ambaye ni Mshindi wa tuzo mbili za Wimbo Bora wa Hip Hop kupitia wimbo
wake wa Mathematics na Tuzo ya Msanii bora wa Hip Hop, alishambulia
jukwaa huku viitikio vyake vikiimbwa na DJ Choka.
Wasanii
hao wiki ijayo wanataraji kutoa burudani kama hiyo jijini Mbeya katika
uwanja wa Michezo wa Sokoine na tayari walisha tumbuiza na kuwashukuru
mashabiki wao wa Mkoani Dodoma na Jijini Mwanza.









No comments:
Post a Comment