TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Tuesday, 24 April 2012

TEWUTA IMEWATAKA TCRA KUPUNGUZA TOZO INAYOLIPWA NA MAKAMPUNI YA SIMU NCHINI.



(NA VERONICA KAZIMOTO – MAELEZO)
DAR ES SALAAM

 Chama cha Wafanyakazi wa Sekta ya Huduma za Mtandao wa Mawasiliano Tanzania (TEWUTA) kimeitaka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TICRA), kupunguza tozo inayolipwa na makampuni ya simu nchini.
 
Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dare s Salaam leo, Katibu Mkuu wa chama hicho Junus Ndaro amesema TCRA imeshindwa kusimamia na kuhakikisha gharama za huduma za mawasiliano ya simu zinapungua na kuwa na uwiano sawa kwa tozo za makampuni yote Tanzania.
 
“Mamlaka imeshindwa kuwaeleza watanzania kwa uwazi na huku ikitambua kuwa moja ya jukumu lake ni kupanga bei elekezi kwa makampuni ya simu, kitendo ambacho hakijafanyika toka mamlaka hiyo iundwe na kutangazwa kwenye vyombo vya habari”, amesema Ndaro.
 
Ameongeza kuwa pamoja na mambo mengine chombo hiki kiliundwa kwa madhumuni ya kumsaidia mteja kupata bei nafuu kila anapotumia mtandao wowote wa simu.
 
“Ni ukweli kuwa watanzania wamechoka kutembea na simu zaidi ya moja za mitandao tofauti kwa sababu ya kutafuta punguzo kwa mtandao husika, hivyo ni wajibu wa TCRA kusimamia mitandao yote ya simu nchini kuwa na bei zenye uwiano wa karibu” amesisitiza Ndaro.  
Ndaro amesema kuwa serikali imeleta Mtandao wa Mkongo (FIBRE) ambao gharama zake za uendeshaji ni mdogo sana na unafanya kazi vizuri kwa haraka zaidi hivyo kuna uwezekano mkubwa kwa TCRA kupunguza gharama wanazotoza kutoka kwenye makampuni ya simu.
You might also like:

No comments:

Post a Comment