TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Tuesday, 24 April 2012

CUF yalalamikia polisi Tandahimba

Peter Mwenda
CHAMA cha Wananchi (CUF) kimesikitishwa na vitendo vya kikatili vilivyofanywa na Jeshi la Polisi dhidi ya wananchi wa Tandahimba.

Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba akizungumza jana Dar es Salaam kuhusiana na tukio hilo alisema ajali ya moto iliyotokea Aprili 17 mwaka huu na kusababisha maduka 55 kuteketea, gari na pikipiki pamoja na ofisi ya Mkuu wa Polisi wilaya ya Tandahimba kuwa ajali hiyo inahusishwa kuwa polisi ndiyo wanadaiwa kuchoma.


Alisema inashangaza kuhusiana na jeshi la polisi badala ya kulinda amani na kuzuia vitendo vya uhalifu wanadaiwa kutenda makosa hayo.

"Siku ya tukio polisi walikuwa ndani ya ofisi ya OCD na kinachotushangaza katika tukio hakuna majivu ya makaratasi yaliyoungua wala hakuna samani iliyotangazwa" alisema Profesa Lipumba.

Alisema sababu za kulituhumu jeshi hilo kuhusika siku ya ajali ni kuwa walinzi na wananchi wa eneo hilo walikatazwa kwenda kusaidia kuzima moto.

Pia kinachoshangaza kingine ni kuungua kwa baadhi ya maduka ambayo wanadaiwa kuwa ni wafuasi wa CUF pekee na kuacha mengine ambao ni wafuasi wa CCM.

Alisema kutokana na hali hiyo CUF imetoa msimamo kwa kuitaka Serikali kuwajibika kwa hasara zilizojitokeza na kulipa fidia kwa watu walioumia kwa risasi na vipigo katika operesheni hiyo ya kikatili dhidi ya wananchi.

Profesa Lipumba alisema serikali ilipe wafanyabiashara wote waliopoteza mali na majengo yaliyoharibiwa, serikali iwafute kazi na kuwafikisha mahakamani askari wote waliohusika na tukio hilo kwa kuwa wanafahamika.

Alisema CUF inaitaka Serikali imfukuze kazi Mkuu wa wilaya ya Tandahimba kwa kushindwa kuongoza na kuwaeleza wananchi ukweli kuhusu namna Serikali inavyoshughulikia tatizo la malipo ya pili ya korosho.

Tume ya haki za binadamu ifanye uchunguzi wa kubaini haki za binadamu na kuwawajibisha wahusika na kupendekeza hatua za kuchukua ili hali hiyo isijirudie katika maeneo mengine.

Aprili 11 wananchi wa Tandahimba walifanya maandamano ya kudai malipo ya pili ya korosho ambapo baadhi ya wakulima waliweka magogo barabarani katika mazingira hayo polisi iliwatawanya kwa kuwapiga risasi za moto na kuwakamata vijana 50.

mwisho

No comments:

Post a Comment