Na Mwandishi Wetu
MTANDAO wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) limesikitishwa na kifo cha Charles Kanumba kilichotokea jana alfajiri nyumbani kwake Sinza, Vatican baada ya kutoka mtafaruku na mpenzi wake Lulu.
Mwenyekiti wa SHIWATA, Caasim Taalib na uongozi mzima wamtandao huo ambako Kanumba alikuwa mwanachama ambaye alishiriki uundwaji na uanzishwaji wa kijiji cha wasanii Mkuranga, umeupokea msiba huo kama pigo kubwa katika harakati za wasanii kuungana pamoja kutafuta njia ya kukomboa maisha yao.
Taalib alisema SHIWATA inatarajia kufanya kikao cha dharura cha kuona jinsi watakavyoshiriki msibba wa Kanumba ambaye ameacha simanzi kubwa kwa watanzania wa rika zote, watoto, wazee na vijana ndani nha nje ya tanzania ambako alionesha umahiri wake katika filamu.
mwisho
No comments:
Post a Comment