TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Tuesday, 24 April 2012

Mkutano Mkuu ALAT Mei3-5 Dar

Na Peter Mwenda

JUMUIYA ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) imeandaa mkutano wa 28 wa mikakati ya kuweka ubia baina ya sekta ya umma na sekta binafsi.

Mwenyekiti wa ALT, Dkt. Didas Masaburi akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana alisema mkutano huo utakaofanyika Dar es Salaam Mei 3-5,Dar es Salaam mgeni rasmi atakuwa Rais Jakaya Kikwete.

Dkt. Masaburi alisema hiyo ni fursa ya pekee kwa sekta binafsi, taasisi za Serikali na mashirika ya umma kushiriki pamoja na viongozi, watendaji wa serikali za mitaa kujadili mambo yanayowakwamisha kushindwa kuwajibika.

Alisema kwa kuwa Serikali za mitaa zinakabiliwa na changamoto mbalimbali hasa na kushindwa kukusanya mapato na halmashauri nyingi kushindwa kuweka mahesabu yao sawa sawa mkutano huo utapata fursa ya kutafuta njia ya kuondoa matatizo hayo.

Alisema ALAT itapendekeza kuongezwa kwa fedha za madiwani ili wawajibike ipasavyo kutoka sh. 120,000 wanayolipwa sasa kufikia sh. 500,000 kwa mwaka.

Dkt. Masaburi alisema mbali ya kualika viongozi mbalimbali mashuhuri ALAT imemwalika Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Bw.Ludovick  Utouh na viongozi wengine wanahusika na serikali za mitaa.

Alisema katika mkutano huo utakaohudhuriwa na washiriki 500 ambao ni mameya na wenyeviti wa majiji, manispaa, wilaya, wakurugenzi na wabunge mmoja kutoka kila mkoa.



No comments:

Post a Comment