TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Friday, 6 April 2012

Madiwani CCM, CHADEMA wapanga mikakati Karatu

Na mwandishi wetu,Karatu

SERIKALI ya Tanzania imeshauriwa kuelekezea nguvu vijijini na katika serikali za mitaa ili kufanikisha dhana ya utawala bora. 
 
Ushauri huo ulitolewa jana katika warsha ilifanyika katika ukumbi wa Kanisa la Kilutheri la Kiinjili (KKKT)Karatu uliandaliwa kwa ushirikaino wa Shirika la Konrad Adenauer Stiftung (KAS) kutoka Ujerumani na Halmashauri ya Mji wa Karatu.

Katika majadiliano hayo ambayo pia yalikuwa na lengo la kutafuta namna ya kuleta maendeleo katika jimbo la Karatu ambalo madiwani wake wanatoka vyama vyenye itikadi tofauti, kauli mbiu ya warsha hiyo ilikuwa "Ufanisi Katika Serikali za Mitaa-Uwajibikaji na Ushirikiano.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Karatu Bw. Lazaro Massay, mwakilishi wa Afrika na Mashariki ya Kati, Bw. Peter Girke na Bw. Stephan Reith mwakilishi mkazi wa KAS nchini Tanzania, warsha hiyo, lengo la warsha hiyo lilikuwa kuondoa tofauti za kiitikadi katika utendaji kazi, kuleta ushirikiano na kupanga mikakati ya kuleta maendeleo kwa pamoja.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Karatu Bw. Clement Berege, aliongoza mdahalo huo akisaidiwa watendaji wa tarafa na kata katika halmshauri hiyo katika mijadala iliyofanyika ni kufanikisha mawasilaino kati ya watendaji katika ngazi mbali mbali tokea vijijini, kata, tarafa na wilaya. 

Miongoni mwa mambo yaliyolalamikiwa na wanawarsha hao ni tatizo la urasimu na kwamba wao hawana mamlaka ya kuchukua maamuzi muhimu isipokuwa wanatakiwa wapeleke maombi wizarani kisha ndipo wapate kibali cha kuchukua uamuzi wowote. Wanawarsha walidai jambo hilo linachelewesha maendeleo,
 
Mtoa mada katika warsha hiyo Bibi Anna Mghwira ambaye mhadhiri Chuo Kikuu cha Makumira ambaye alizungumzia mada tatu tofauti ya kwanza ikiwa ni kufanya kazi kwa ushirikiano (timu) na uwajibikaji kwa lengo la kufanikisha uongozi.

Karatu ilichaguliwa kutokana na ukweli kwamba halmashauri hiyo inaundwa na madiwani wa vyama viwili tofauti, Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo  (CHADEMA) chenye madiwani wengi katika halmashauri hiyo.  
 

"Katika mazingira yenye uhaba wa raslimali ushirikiano ni jambo la muhimu sana hivyo mnatakiwa kuweka tofauti za itikadi zenu pembeni ili muweze kusonga mbele"alisema Bibi Anna.


Aliwashauri viongozi hao kusoma na kuyatumia mabadiliko mbali mbali ya serikali za mitaa kwa lengo la kurahisisha maendeleo mingoni mwao na kuongeza kuwa kama serikali za mitaa zitafanya hivyo zitakuwa zimeipunguzia mzigo serikali kuu. 

Serikali za mitaa zinakabiliwa na changamoto mbali mbali ambazo zinadaiwa kukwamisha maendeleo kama vile kutokuwa na ruhusa ya kuajiri wafanyakazi wapya na haziruhusiwi kuwafukuza kazi wale walioshindwa kuwajibika hali hii imesababisha watendaji wengi kutokuwa na nidhamu inayostahili. 

Mwisho 

No comments:

Post a Comment