Bia
ya Ndovu Special Malt inayotengenezwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia
Tanzania (TBL), imedhihirisha ubora wake kimataifa baada ya kushinda kwa
mara nyingine tena tuzo ya dhahabu yenye hadhi ya juu zaidi ya ubora wa
bidhaa kimataifa ijulikanayo kama “Grand Gold Quality Award”
Akizungumza
na waandishi wa habari, meneja wa Bia ya Ndovu Bi. Pamela Kikuli
alisema; Tunayo furaha kubwa sana kuwajulisha wadau wa Bia hii ya Ndovu
Special Malt juu ya ushindi huu mkubwa ambao Bia hii imenyakua katika
tuzo za bidhaa za kimataifa zinazotolewa na Taasisi ya kimataifa
inayoangalia ubora wa bidhaa ya “Monde Selection International Quality
Institute” iliyopo Brussels, Ubelgiji (Belgium). Tuzo hii yenye hadhi ya
juu kabisa katika ubora wa bidhaa kimataifa inajulikana kama “Grand
Gold Quality Award” na hushindanisha bidhaa toka Mataifa mbalimbali
ambapo mwezi huu Aprili taasisi hiyo imetangaza rasmi kuwa “Ndovu
Special Malt” imeshinda tena tuzo ya “Grand Gold” kwa mwaka 2012.
Alisema Pamela.
Akizungumzia
Ubora wa bia ya Ndovu Special Malt, Mpishi mkuu wa Bia wa TBL Bwn.
Gaudence Mkolwe alisema; Tunakumbuka kuwa mwaka 2010 Bia hii ya Ndovu
Special Malt ilishinda kwa mara ya kwanza tuzo hii ya Grand Gold ikiwa
na umri wa miezi tisa tu sokoni toka ibuniwe, na kuweka historia kwa
nchi yetu kuwa ndio Bia ya kwanza kushinda tuzo hiyo hapa Tanzania, na
leo Bia ya Ndovu Special Malt inawadhihirishia wadau wake na watanzania
wote kwa ujumla kuwa imeendeleza ubora wake kitaifa na kimataifa hadi
kupata tuzo hii kwa mara ya pili. Haya ni mafanikio makubwa na ya
kujivunia si tu kwa wapenzi wa Bia hii, bali kwa Taifa zima kwa kuwa na
bidhaa zinazotingisha anga za kimataifa kwa Ubora, na ukizingatia kuwa
Bia hii imebuniwa na watanzania na inatengenezwa na watanzania. Haya ni
mafanikio makubwa ya kujivunia.
Nae
Meneja wa miradi maalum na Mawasiliano wa TBL Bi. Emma Orio alitoa
utaratibu wa upokeaji wa tuzo hizo; Tuzo hizi za mwaka 2012,
zitakabidhiwa rasmi mwezi Juni 2012 katika hafla kubwa iliyoandaliwa
huko Athens, Ugiriki na kufuatiwa na hafla mbalimbali zitakazofanyika
hapa nyumbani mara tu tuzo hii itakapowasili nchini. Tunawapongeza
wapenzi wote wa Bia hii ya Ndovu Special Malt, kwa kufanya chaguo sahihi
kwa kutumia Bia inayoongoza kwa ubora wenye hadhi ya juu na tunawaahidi
kuendelea kuwapatia ubora huu siku zote. Alisema Bi. Emma.
You might also like:
No comments:
Post a Comment