TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Tuesday 13 March 2012

Mtanzania awa Balozi wa kuwakilisha Mexico nchini

Na Peter Mwenda

SERIKALI ya Mexico imefungua ubalozi mdogo nchini ambako mtanzania Bw. Mohammad Reza Saboor amekuwa Balozi wa mdogo wa Kwanza kutunukiwa heshima hiyo.

Akifungua ubalozi huo jana Dar es Salaam, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Bernard Membe alisema hatua hiyo ni heshima kubwa kwa Tanzania kupata ubalozi mdogo ambao utaongozwa na mtanzania.

Alisema uhusiano wa Tanzania na Mexico ulikuwepo kutoka zamani na kuahidi kuwa ubalozi huo utaongeza ushirikiano katika sekta mbalimbali za kuleta ushirikiano wa nchi hizo mbili.

Balozi wa Mexico anayewakilisha nchi za Afrika Mashariki Bw.Luis Javier Campuzano alisema ushirikiano wa nchi mbili hizo ulianza miaka ya 1970 wakati wa Rais wa Kwanza wa Tanzania Julius Nyerere kutembelea nchi yake na Rais wa Mexico wakati huo Bw. Luis Echeverria kufika Tanzania.

Alisema anatoa nafasi kwa watanzania kujenga ushirikiano na urafiki katika ujenzi wa nyumba, maendeleo ya kilimo cha mahindi, uhifadhi na kujenga uhusiano wa kielimu ya sekondari na Vyuo Vikuu.

Balozi Luis alisema Bw. Reza ambaye atakuwa Balozi wa Heshima wa Mexico nchini pia utachangia kujenga uhusiano kati ya nchi mbili kujenga utamaduni, elimu, ufundi, biashara na uwekezaji.

Balozi wa Heshima Bw. Reza alisema amepokea jukumu hilo akiamini kufanya kazi kwa utiifu na kukuza ushirikiano uliokuwepo kati ya Mexico katika kukuza zao la katani ambalo Tanzania linastawi katika mikoa ya Tanga na Morogoro.

mwisho

No comments:

Post a Comment