Na Mwandishi Wetu
NAIBU Waziri wa Ujenzi, Dkt. Harrison Mwakyembe ameanza kazi rasmi leo huku akisema ugonjwa wake unaomsumbua utajulikana baada ya Serikali na Jeshi la Polisi Tanzania kumaliza utafiti.
Pia amemshukuru Rais Jakaya Kikwete, watanzania na wananchi wa jimbo lake la uchaguzi la Kyela Mkoani Mbeya kumuombea mungu wakati anaumwa.
Alisema sasa huko fiti na mafaili lundo aliyoyakuta mezani kwake ameanza kuyafanyia kazi na kutoa shukurani kwa Waziri wake, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kufanya kazi peke yake katika kipinbdi chote alichukua akiumwa na kutibiwa kwenye hospitali ya Appolo, India.
Dkt. Mwakyembe ambaye chanzo cha ugonjwa wake kinasadikiwa kuwa alilishwa sumu bado taarifa ya ukweli kuhusu tuhuma hizo zimebaki mikononi kwa Serikali na Jeshi la Polisi Tanzania.
mwisho
No comments:
Post a Comment