Na Peter Mwenda
RAIS Jakaya Kikwete amevitaka vyama vya Ushirika kuacha tabia ya kuuza majengo yao na kuajiri watendaji wenye sifa.
Akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Ushirika duniani jana Rais Kikwete alisema vyama vya ushirika vilichangia kujenga uchumi imara na kusomesha wasomi ambao waliwahi kuwa maprofesa na mawaziri nchini.
Rais Kikwete alisema baadhi ya wasomi hao ni Bw. George Kahama walianzisha chama cha Ushirika mkoa wa Kagera mwaka 1941 na kusomesha wasomi wengi nchini.
Alisema miaka kumi baada ya uhuru vyama vya ushirika vilichanua na kutoa mchango mkubwa kwa serikali lakini baada ya hapo vilianza kufa kimoja hadi kingine.
Alisema Vyama cha Kuweka na Kukopa (SACCOS) vimeanza kuimarika na kuongeza mtaji wao kufikia Bil.529.6 ambazo zinatosha kuanzisha benki yao itakayowakopesha wafanyakazi na wakulima katika kukuza kilimo.
Alisema benki ya CRDB ambayo ilianzishwa kwa ajili ya wakulima ilibinafsishwa na kuleta maendeleo ambayo yanafaa kuigwa kwenye benki mpya ya ushirika.
Rais Kikwete alikipongeza Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania (TFC) wanaojenga nyumba ya ghorofa 20 itakayokuwa jengo pacha ya jengo la Ushirika Mnazi Mmoja.
Alisema ushindani wa kujenga majengo ya kisasa unachangia kuleta maendeleo na kuongeza kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambacho yeye ni Mwenyekiti wake kinajenga nyumba ya ghora 35 katika eneo lao la Sukita.
mwisho
No comments:
Post a Comment