TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Tuesday, 8 November 2011

Tanzania mwenyeji nchi zinapambana ya ujangili

Na Peter Mwenda

WIZARA ya Maliasili na Utalii ni mwenyeji wa mkutano wa kumi wa Baraza la Mawaziri wa nchi wanachama wa Mkataba wa Lusaka wa kushirikiana katika mapambano ya kuzuia biashara haramu ya wanyamapori na mimea.

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori nchini, Bi. Nebbo Mwina alisema mkutano huo utafanyika kuanzia leo Dar es Salaam utashirikisha nchi saba wanachama na tatu washiriki utajadili mbinu mbalimbali za kisasa za kupambana na majangili.


Alisema katika mkutano huo ambao mada kuu itakayotolewa na Profesa Pius Yanda wa Chuo Kikuu cha dar es Salaam itahusu changamoto na fursa ya uhifadhi wanyamapori barani Afrika na kuongeza ushirikiano na utengamano, utainushaisha Tanzania kupambana na ujangili.

Bi. Mwina alisema mkutano huo unafanyika wakati changamoto za ujangili na biashara haramu ya wanyamapori hasa tembo na faru zimeongezeka katika bara la Asia ppia utatoa maamuzi muhimu yatakayoboresha utekelezaji wa mkataba.

Alisema nchi wanachama watakaohudhuria mkutano huo ni Congo (Brazzaville),Kenya, Lesotho, Liberia, tanzania, Uganda na Zambia na nchi za Ethiopia, Afrika Kusini na Swaziland ni washiriki ambao bado hajaridhia mkataba huo.

Bi. Mwina alisema mkutano huo ambao Mwenyekiti wake ni Waziri wa Maliasili na Utalii wa Tanzania,Bw. Ezekiel Maige utapitia taarifa ya mapendekezo ya utekelezaji wa kikosikazi cha mkataba wa Lusaka.

Mawaziri watakaohudhuria ni Waziri wa Nchi wa Utalii, Wanyamapori na Urithi wa Jamhuri ya Uganda, Bi. Agnes Enguyu,Waziri wa Maendeleo Endelevu,Misitu,Uchumi na Mazingira wa Congo, Bw. Henri Djombo.

Wengine ni Waziri wa Misitu na wanyamapori wa Jamhuri ya Kenya, Dkt. Noah Wekesa na Naibu Waziri wa Madini na Maliasili wa Jamhuri ya Zambia, Bw. Richard Musukwa.

Mkurugenzi wa Kikosikazi cha Azimio la Lusaka, Bw. Bonaventure Ebayi alisema ushirikiano huo umesaidia kupunguza ujangili na maliasili nyingi zimekamatwa kwa wananchi wanachama kulinda mali zao.

mwisho

No comments:

Post a Comment