TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Thursday, 27 October 2011

Zitto Mahututi Muhimbili,afya yake yazorota

Na Peter Mwenda

PILIKAPILIKA zilitawala hospitali ya Taifa ya Muhimbili jana baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, POAC) Bw. Zitto Kabwe kupelekwa katika chumba cha wagonjwa wenye uangalizi maalum, (ICU) baada ya kuzidiwa na homa.

Mpaka saa 12 jioni ya jana, Mwandishi wa habari hizo alifika Muhimbili na kuwakuta watu kibao wakiwemo ndugu zake wakitaka kuingia wodini kupata ukweli kuhusu afya ya Zitto ambaye alivumishwa pia kufariki dunia.

Ililazimika Katibu wa Bunge, Bw. Thomas Kashilila kufika Muhimbili na kutoa ufafanuzi wa afya ya Bw. Zitto kuwa hajafa na hali yake si mbaya kwani kinachomsumbua kwa sasa ni kichwa kuuma.

"Hali ya Mh. Zitto si mbaya na yupo hai isipokuwa anaendelea na matibabu kwa vile homa zinapanda mara kwa mara, madaktari wanafanya utaratibu wa kumpeleka India lakini ni mwishoni mwa wiki na huenda ikawa wiki ijayo" alisema Kashilila.

Uvumi wa kifo cha Zitto haupo na Bw. Kashilila alifanya naye mazungumzo hadi jana saa 12 jioni lakini kutokana na ushauri wa madaktari wameomba apumzike inawezekana hali hiyo ndiyo iliwafanya watu wavumishe.

mwisho

No comments:

Post a Comment