TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Thursday, 13 October 2011

wanawake wanajeshi (JUMAWAMA) kupata mkopo mil. 5/-bila dhamana

Na Peter Mwenda

MKURUGENZI Mtendaji wa Benki ya Wanawake Tanzania (TWB) Bi. Magreth Chacha amewataka wanachama wa Kikundi cha Jumuiya ya Maendeleo ya Wanawake (JUMAWAMA) watambue kuwa ili kupata mafanikio katika shughuli za ujasiriamali ni lazima wajifunze kuweka akiba.

Akifungua semina ya siku moja ya ujisiriamali juzi, Bi. Chacha alisema bila kutunza akiba wanachama wa kikundi hicho watashindwa kuendesha shughuli za ujasiriamali za ufugaji, usindikaji wa matunda, utengezaji wa mishumaa na shunghuli nyingine zinaziofanywa na akinamama hao.

Alisema kikundi cha JUMAWAMA ni mfano wa kuigwa na akinamama wengine akisisitizawajitahidi kutafuta nafasi ya kutafuta maendeleo huku akiwaahidi kukitafutia uhusiano na nchi nyingine za nje ili kupata elimu zaidi ya ujasilimali.

Bi. Chacha alisema mikopo inayotolewa na TWB inayofikia sh. mil. 2 kwa kila mwanachama bila dhamana inatarajia kuongezeka kufikia sh. mil. 5 endapo Bodi ya Benki hiyo itaridhia.

Alisema michango ya Kicheni Pati iangalie mitaji na kuona kama kuna akiba ya kutosha vingenevyo husababisha wanawake wengi kujikuta hawana misingi ya kuendesha biashara zao kwa ajili ya kutoa michango na kujikuta anadaiwa fedha.

Mwenyekiti wa JUMAWAMA, Bi. Salma Omari alisema kikundi hicho ambacho kinaundwa na wake wa wanajeshi waliopo kazini na waliostaafu wapatao 350 kinatarajia kufunga kuku wa mayai ya kienyeji katika eneo lao la ekari 200 lililopo Bagamoyo.

Bibi. Salma alisema katika mradi huo wanatarajia kuuza mayai na kuku kwa wateja katika hoteli za kitalii na watu binafsi baada ya kupata mafunzo ya ufugaji wa kuku kutoka katika kituo cha Dar es Salaam Trainging Ventures ambako kila mwanachama aliyepata mafunzo hayo alipata rizuku ya vifaranga 100.


Bw. Salma alisema umoja huo uligawanywa katika vikundi kumi ambako kila kimoja kina wanawake 40 ili kurahisisha kutatua matatizo madogo yanayohusiana na kikundi cha JUMAWAMA.

No comments:

Post a Comment