TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Friday, 9 September 2011

Mgombea CUF amshambulia Rostam Azizi

Na Peter Mwenda, Igunga
MBUNGE wa zamani wa Jimbo la Igunga Bw. Rostam Aziz ameshushiwa lawama kuwa aliitenga Tarafa ya Igurubi ambayo ndio pekee isyokuwa na maendeleo na huduma muhimu ya umeme katika Jimbo zima la Igunga.
Mgombea wa CUF Leopold Mahona akihutubia mkutano wa hadhara katika Tarafa hiyo jana, alisema Rostam aligoma kupeleka umeme, kuchimba visima vya maji na kuwakwamua wananchi wa eneo kielimu.
Alisema Igurubi inakabiliwa na matatizo mengine mbalimbali likiwamo daraja la kuwaunganisha na Tarafa nyingine ya Mbutu, ubovu wa barabara na kushindwa kuweka zao la pamba katika mfumo ambao unaweza kuwanufaisha wananchi kama ilivyo mkoa wa Shyinyanga.
“Igunga ndio wilaya pekee inayozalisha pamba kwa wingi lakini cha kushangaza bei yake ni chini ya Sh 1000 kwa kilo wakati Shinyanga bei yao ipo juu ya Sh. 1000 kwa kilo,” alisema Mahona.
Mahona alibainisha pia kwamba wilaya hiyo inakabiliwa na tatizo kubwa la mifugo ambapo hadi sasa hakuna malambo wala majosho ya kuoshea mifugo hatua ambayo imesababisha maisha ya wananchi wa Kata hiyo kuwa magumu.
“ Nikichaguliwa kuwa mbunge naomba mnipatie siku 400 tu ambazo nitahakikisha matatizo yote yanamalizika.
“Kamwe sintafanya kama walivyofanya viongozi waliopita akiwa Benjamini Mkapa, Edward Lowassa, Rostam na hawa waliopo sasa akiwamo Pinda, Kikwete ambao wameshindwa kujenga daraja la mto Mbutu,” alisema Mahona na kuongeza:
“ Mwaka 2006 nilipoteza ndugu wawili kwenye daraja hilo ambao walizolewa na maji, sasa kilio hiki kitafikia mwisho Oktoba 2 siku mtakayonichagua kuwa mbunge wenu,” alisema.
Mahona aliendelea kubainisha kwamba Rostam kupitia CCM aliwabebesha gunia la misumari wananchi wa Igunga hususani Tarafa ya Igurubi kwani maisha ya wananchi yamekuwa magumu na yanaendelea kuwa duni kila siku kwa sababu ya sera kandamizi za CCM.
“Nyinyi mmeuzwa sasa mimi nimekuja kuwakomba kama ndugu yenu ambaye ni mzaliwa wa jimbo hili, nikiwa mgombea pekee mzaliwa kati ya tuliopo.
“Mwaka jana nilighombea nafasi hii lakini miliona Rostam anafaa zaidi, safari hii naomba kura zenu ili nirudishew hadhi ya wananchi wa Igunga, jimbo lenye utajiri mkubwa  kati ya majimbo ya mkoa wa Tabora,” alisema Mahona. 
 Alisema mfano wa utajiri huo ni kitendo cha hivi karibuni ambapo baadhi ya vijana waliokota maadini ya almasi barabarani kitendo ambachio kinaonyesha kuwa ardhi yote ya Igunga imebarikiwa.
Alisema endapo akichaguliwa kuwa mbunge atahakikisha anaanzisha Chuo cha mafunzo ili vijana wanaomaliza darasa la saba na kidato cha nne na kushindwa kuendelea watapatiwa mafunzo stadi kwa ajili ya kuendesha maisha yao katika ajira zisizo rasmi.
“ Nitahakikisha ninajitahidi kujenga nyumba za walimu kwenye shule zetu zilizopo ili walim,uwa wanaopangiwa kuja kufundisdha watoto wetu waishi maisha yanayofanana na wale wanaopangiwa katika mikoa mingine nchini.
Mwisho.  

No comments:

Post a Comment