TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Tuesday, 6 September 2011

Maalim Seif aingia Igunga

Na Peter Mwenda, Igunga
MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar,Maalim Seif Hamad a ameitaka Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Igunga kuacha kuingilia shughuli za uchaguzi katika kipindi hiki cha uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga.
Akizungumza na Kamati ya Ulinzi ya Wilaya ya Igunga ambayo Mweenyekiti wake ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Bibi Fatuma Kimario,Maalim Seif alisema kamati hiyo ihakikishe kuwa vyombo vya ulinzi na usalama haviingilii uchaguzi huo wala kupendelea chama cha siasa.
Alisema vyama vya siasa viachiwe vijinadi bila kuingiliwa ili atakyechaguliwa kuwa mbunge wa Igunga atokane na kura halali za wananchi wa jimbo la Igunga.
"Siasa ni hisia hivyo wito wangu hasa tusizipe nafasi hisia zetuzisitokee kabisa kama mtasimamia shughuli zenu bila upendeleo hatimaye tutampata mbunge ambaye tunataka achaguliwe kwa taratibu za uwazi kabisa na maamuzi yafanywe na wananchiƔlisema Maalim Seif.
Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar ambaye pia ni Katibu Mkuu wa chama cha Wananchi CUF alisema wakati mwingine uchaguzi unapomalizika utata unajitokeza wa kujumlisha kura na kutumika nguvu ambazo hazistahili kutumika,wakati mwingine wasimamizi wanapokuja na matokeo yao kutoka kata wanakuta matokeo mengine ambayo hayapo.
Alisema Tanzania nzima inaangalia uchaguzi wa Igunga na kumtaka Mkuu wa wilaya kuwa makini na kuvitaka vyama vya siasa walivyoweka wagombea wa ubunge katika jimbo hilo vifuate ratiba zao bila kuingiliana na kuacha vurugu.
"Ukiona hapa mwenzako yupo na wewe ni zamu yako kufanya mkutano hakuna haja kugombana,tumepangiwa utaratibu wadau wote tufuate, tushirikiane kuondoa kasoro hizo"alisema Maalim Seif.
Katika ziara ya Makamu wa Rais Zanzibar, aliyefuatana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora,Bw. Abedi Mwinyimsa alipokea taarifa fupi za wilaya ya Igunga na kufanya kikao cha ndani na viongozi wa CUF waliopiga kambi Igunga kabla ya kuanza kampeni za ubunge.
Awali Mkuu wa Wilaya,Bibi Kimario alisema wilaya ya Igunga inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wa chakula.
CUF imemsimamisha Bw.Leopold Mahona kugombea kiti cha Ubunge katika jimbo hilo lililoachwa wazi na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo, Bw.Rostam Aziz (CCM) aliyejiuzulu nyadhifa zake katika chama hicho.
Vyama tisa vya siasa vimewasimisha wagombea,chama cha CHAUSTA kimemsimamisha Bw. Hassan Ramadhani, Bw. Hemed Ramadhani (UPDP),John Magona (SAU),Dkt. Kafumu Dalaly (CCM).Chadema, Bw.Joseph Kashindye,Bw.Steven Mshuyi wa AFP,Bw. Lazaro Ndegeya (UMD) Bw. Said Cheni (DP).Kampeni za uchaguzi huo zinaanza leo katika kata 26 za Jimbo la Igunga mkoani Tabora.

No comments:

Post a Comment