Na Peter Mwenda, Igunga
CHAMA cha Wananchi (CUF) kimelitaka Jeshi la Polisi kumkamata Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana (UVCCM) Bw. Martin Shigela na kumchukulia hatua za kisheria kwa kosa la msafara wake kumpiga mateke na kumuumiza Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazee wa chama hicho tawi la Iyogelo kata ya Kining'ilila, Bw. Salum Masanja (55) aliyelazwa katika hospitali ya wilaya ya Igunga.
Kaimu Katibu Mkuu wa CUF Bara, Bw. Julius Mtatiro alisema jana kuwa kama hatua ya kumkamatana Bw. Shigela haitafanyika chama chake kitajibu mapigo na kuanza kuchukua hatua ya kuwashughulia CCM kwa kuwapiga kila kona wanapokutana nao.
"Kama polisi ikiwaacha CCM waendelee kupiga watu wetu na sisi tutaanza kuwapiga, waliompiga na kumuumiza kiongozi wetu wanajulikana ni Bw. Shigela anajulikana sana,tunataka polisi wachukue hatua wakishindwa tutawasaidia"alisema Bw. Mtatiro.
Alisema tukio la kupigwa Mwenyekiti wa wazee wa CUF kulisababishwa Mwenyekiti wa UVCCM, Bw. Shigela akiwa na magari matatu ya CCM walifika kijiji cha Iyogelo na mkukuta Bw. Masanja akipandisha bendera ya CUF nyumbani kwake na kumtaka ateremshe bendera kwa madai walikuwa wafanye mkutano hapo.
Kaimu Katibu huyo alisema katika kampeni za uchaguzi Igunga endapo kila mtu akiachwa apige watu huku wakiachwa bila kuchukuliwa hatua basi hakutakuwa na uchaguzi Igunga wa amani na kuonya kuwa CCM iache mara moja tabia hizo kwa sababu itasababisha hatari.
Alisema kiongozi wao huyo tangu afikishwe hospitalini hapo juzi jioni hakupatiwa msaada wowote wa matibabu hadi jana mchana ambako viongozi wa CUF walipofika kumuona.
Bw. Mtatiro alisema inakuaje kijana wa CCM aliyemwagiwa tindikali kupewa huduma na matibabu haraka lakini wa CUF anashindwa kupewa huduma stahili kwa saa 18 zilizopita bila hata panado.
Akizungumza katika hospitali ya wilaya, Bw. Masanja alisema anasikia maumivu makali kwenye mbavu na kichwani baada ya kupigwa mateke na watu watatu walikouwa wamevaa nguo za kiraia waliofuatana na Bw. Shigela aliyekuwa katika msafara wa magari matatu yenye bendera za CCM.
Bw. Masanja alisema baada ya kugoma amri ya kushusha alijikuta akipigwa ngwara na kuanguka kulikofuatiwa na mateke mbavuni, kichwanina kupoteza fahamu na kuzinduka baada ya saa moja.
Bw. Masanja alisema alifikishwa hospitalini hapo na polisi lakini hakupata hata vidonge vya kutuliza maumivu wala daktari kumchunguza afya yake wakati bado akiendelea kusikia maumivu makali.
Mgombea ubunge Jimbo la Igunga wa CUF, Bw. Leopold Mahona amelaani vikali vitendo cha kupigwa wanachama wake wanaompigia debe achaguliwe kuwa mbunge.
Akizungumza katika mkutano wa kampeni juzi katika kijiji cha Nyandekwa,Bw. Mahona alisema kitendo hicho kitaamsha hasira za kufanya uchaguzi usiende kama ilivyotarqajiwa.
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi na Kamanda wa FFU, Bw. Telesfory Anaclet alisema CUF haipaswi kulaumu jeshi hilo kwa kushindwa kumkata Katibu Mkuu wa UVCCM kwa sababu taarifa za awali na maelezo ya mlalamikaji alimtaja Bw. Shigela lakini hakufafanua mtu huyo ni Katibu Mkuu wa UVCCM.
Alisema jeshi la polisi lilitoa ushirikiano mkubwa kwa sababu baada ya kupata taarifa ya tukio hilo alituma askari wa kwenda kumchukua majeruhi na kumwandikia PF3 na kumfikisha hospitali.
Kamanda Anaclet alisema kumekuwa na matukio ya uhalifu na kusababisha majeruhi, mashambulio ya kudhuru mwili na kudhalilisha zinazodaiwa kuwa ni siasa au sehemu ya kampeni.
Alisema hatua za kisheria zitachukua mkondo wake na kuwatqadharisha wananchi kushirikiana kufanyikia kwa uchaguzi wa kumpata mbunge wa Jimbo la Igunga unatarajiwa kufanyika Oktoba 2, mwaka huu.
Akijibu tuhuma hizo Bw. shigela alisema kwanza amesikitishwa na vitendo vya wananchi wa Igunga kupigwa badala ya kuombwa kura kutoka aingie Igunga amekuwa akizunguka kata zote na hakuna sehemu katika matuko kadhaa yaliyojitokeza kutoka kampeni zianze.
Bw. Shigela alisema kutoka afike Jimbo la Igunga hakuna sehemu ambako ameamrisha bendera bendera ya chama chochote cha upinzani ishushwe.
Alisema inawezekana mtu huyo ametumwa azungumze hayo na inawezekana hamjui hata kwa sura ndiyo maana anatamka hayo.
mwisho
No comments:
Post a Comment