Na Peter Mwenda
WAFANYABIASHARA maarufu nchini,Bw. Mustafa Sabodo na Bw. Fidahussein Rashid wametoa msaada wa basi aina ya Eicher lenye thamani ya sh. mil. 60 kwa ajili ya shule ya Sekondari ya wasichana ya Dkt. Asha Rose Migiro ya wilayani Mwanga, Kilimanjaro.
Wakizungumza wakati wa makabidhiano hayo wafanyabiashara hao walisema wataendelea kumuunga mkono Dkt.Asha Rose Migiro katika jitihada zake za kusoma hadi kufikia cheo cha Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Kimataifa.
Waziri Mkuu mstaafu wa Awamu ya Kwanza, Bw. Cleopa Msuya alisema msaada huo utakuwa changamoto kwa wengine kusaidia elimu kwa watoto wa kike ili wafikie hatua ya Dkt. Migiro.
No comments:
Post a Comment