Na Peter Mwenda
NCCR Mageuzi hakitamweka mgombea wa ubunge Jimbo la Igunga katika uchaguzi mdogo badala yake kitasaidia chama chochote cha upinzani kupata kiti hicho.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Katibu Mkuu wa NCCR Mageuzi, Bw. Samuel Ruhuza alisema kuwa wamefikia hatua hiyo baada ya kufanya tathmini katika Kata 26 za jimbo hilo na kubaini kuwa jimbo hilo litachukuliwa na upinzani.
Alisema Sekreterieti ya chama hicho iliyoketi Alhamisi iliyopita iliridhika kuwa NCCR Mageuzi ina mtandao mkubwa katika jimbo hilo.
Alisema katika kikao hicho ambacho yeye ni Mwenyekiti kilipata taarifa kuwa wananchi wa jimbo la Igunga wamekosa imani na CCM hivyo wanataka upinzani uchukue kiti hicho.
Alisema wapinzani wana nafasi kubwa ya kuchukua jimbo hilo ambalo liliachwa wazi na Rostam Aziz (CCM) aliyejivua madaraka hayo na nafasi nyingine katika chama chake.
Bw. Ruhuza alisema NCCR Mageuzi imeamua kuaachia chama kingine kiweke mgombea na wao watashiriki kufanya kampeni kama ilivyowahi kufanya kwa kumwachia Mwenyekiti wa CHADEMA, Bw. Freeman Mbowe baada ya kuona kumweka mgombea wangegawana kura na kuwapa nafasi CCM kuchukua kiti.
Alisema katika jimbo la Tunduru walimuunga mkono mgombea wa CUF na kilimpeleka Mwenyekiti, James Mbatia kusaidia kupigia kampeni pia katika jimbo la Kiteto na jingine la Busanda chama hicho kilifanya hivyo hivyo na hiyo ni kuonesha kuwa chama hicho kinafanya kazi kwa vitendo si maneno ya jukwaani kama wapinzani wengine wanavyofanya.
Alisema wapinzani wakitaka kushinda kiti cha Igunga wamwachia mgombea mmoja na vyama vingine vimuonge mkono na kuona hakuna haja kupoteza muda kugawana kura za wapinzani kwa sababu watanzania wengi wanachoshwa na CCM.
"NCCR Mageuzi tunajitoa mhanga kwa mara nyingine, hatuweki mgombea ubunge Jimbo la Igunga, haina maana kwenda kupeperusha bendera za chama bali tunataka kutumia bajeti yetu ile ile tuliyokuwa tumepanga kusadia upinzani uchukue ushindi.
Alisema NCCR wapo tayari kutoa rasilimali, kutumia muda na gharama kutafuta kiti hicho lichukuliwe na upinzania na kuongeza kuwa wetu wote kuhakikisha upinzani unachukua madaraka ya nchini.
mwisho
No comments:
Post a Comment