TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Wednesday, 31 August 2011

Kamanda Mpinga aonya madereva wasiobadilisha leseni

Na Mwandishi Wetu
KAMANDA wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Bw. Mohamed Mpinga amewaonya madereva wanaokaidi amri ya Serikali ya kubadilisha leseni zao za zamani ili kupata mpya.

Akizungumza na mtandao wa Mwenda Blog, Bw. Mpinga alisema operesheni ya kukamata madereva wasio na leseni mpya inaendelea na watakaobainika watachukuliwa hatua za kisheria.

Alisema mpaka sasa madereva 36 wamekamatwa nchini kote wakiwa hawana leseni mpya na wengine hawajabadilisha leseni zao kwa miaka miwili mpaka miaka mitatu huku wakitembea barabarani bila woga.

Bw. Mpinga alisema kwa mujibu wa takwimu za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Tanzania ina magari 932,749 lakini madereva walibadilisha leseni zao nchi nzima mpaka sasa ni 132,664.

Alisema takwimu hizo zinaimanisha kuwa kuna madereva zaidi ya 800,000 ambao bado hawajabadilisha leseni zao na kuonya kuwa msako wa kila pembe nchini umeanza sambamba na kuchukuliwa hatua za kisheria za papo kwa hapo na kufikishwa mahakamani.

Katika hatua nyingine dereva Issa Ramadhani mkazi wa Tanga aliyesababisha ajali iliyoua wanafunzi 18 wa shule ya sekondari ya Shamsi Maarifa amekamatwa.

Kamanda Mpinga alisema dereva huyo alitarajiwa kufikishwa mahakamani jana kujibu tuhuma za kusababisha vifo vya wanafunzi hao na majeruhi 36 wengine wakiwa ulemavu wa kudumu.

mwisho

No comments:

Post a Comment