TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Monday, 25 July 2011

Nitamkumbuka daima Mwakiteleko tabia ya kujishusha

NA Peter Mwenda

Naibu Mhariri wa NewHabari 2006 Ltd,Danny Mwakiteleko kutoka Februari mwaka 1996 alipojiunga na majira akitokea New Habari akiwa amekuja na rafiki yake mpendwa Jesse Kwayu.

Mwakiteleko aligundua kuwa mtu wa kwanza kuwa rafiki yake nilikuwa mimi wakati huo nikuvuta sigara aina ya Sportsman na yeye akiwa mvutano ya sigara ya SM.

Urafiki huo aliujenga kwa mwandishi mwingine ambaye ni marehemu Conrad Dustan "Mnywambele" au 'Kionambali' na kuunda umoja wetu wa wavuta sigara na wanywaji wa bia aina ya Safari.

Katika kipindi cha miaka minne niliyofanya naye kazi kwa karibu hakuwahi kunivunjia heshima bali aliongeza ukaribu baada ya kugundua nimeoa mke wangu kutoka mkoa wa Mbeya na kuongeza jina akiita shemeji.

Hata wakati akifunga ndoa na mkewe waandishi tuliokuwepo majira wakati huo akina Joseph Kulangwa (Habari Leo),Theophil Makunga Mhariri Mtendaji (Mwananchi), Juma Pinto mmiliki Jambo Leo, Masoud Sanani (Spoti Starehe) na wengine wengi tulishiriki katika harusi yake.

Hata baada ya jopo la waandishi wa majira kuhama kwenda kuanzisha Mwananchi kwenye jengo la CCM mkoa ambako ilipo Redio Uhuru sasa hivi lakini bado marehemu Mwakiteleko nilikutana naye kupata kinywaji.

mwisho

No comments:

Post a Comment