Na Peter Mwenda
KATIBU Mkuu wa Shirikisho la Wasanii Tanzania (SHIWATA), Alex Mwakabana aliyefariki dunia Alhamisi iliyopita baada ya kuugua kwa muda mfupi amezikwa Jumamosi katika makaburi ya mjini Mbeya.
Mwenyekiti wa SHIWATA, Caasim Taalib alisema jana kuwa marehemu Alex alifariki baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa Kisukari ameacha pengo kubwa kwa wasanii wa fani mbalimbali nchini.
Taalib alisema marehemu Alex atakumbukwza na SHIWATA daima kwa ushujaa wake wa kutetea wasanii kama kiongozi na mchezaji maarufu wa sarakasi katika kikundi cha Tiger Acrobatic na Kampuni yake ya Vuvuzela Entertainment ya jijini Dar es Salaam.
Alisema marehemu Alex ambaye ni mmoja kati ya waanzilishi wa SHIWATA alishiriki kikamilifu katika mradi wa wasanii kujiunga na vijiji ili kutekeleza kwa vitendo Sera ya Taifa ya Kilimo Kwanza katika kijiji cha Mwanzega wilaya ya Mkuranga na kijiji cha Visegese kilichopo wilaya ya Kisarawe.
Ibada maalum ya misa ya kumuombea marehemu Mwakabana itafantika Makao Makuu ya SHIWATA katika ukumbi wa Chuo cha Splendid Ilala Jumapili ya Julai 10 kuanzia saa 3 asubuhi.
Alisema SHIWATA iliwakilishwa na wajumbe wawili kutoka makao Makuu jijini Dar es Salaam. Selemani Mchomvu akiongoza msafara huo.
mwisho.
No comments:
Post a Comment