TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Thursday, 21 July 2011

Airtel yagawa madawati kwa shule Mwanza

Na Mwandishi Wetu, Mwanza

KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel imegawa madawati 50 katika shule ya sekondari Kangaye yenye thamani ya sh. mil.3.8 ikiwa ni sehemu ya shughuli zao za kusaidia jamii.

Meneja Biashara Kanda Ziwa  Bw. Ally Maswanya alisema Airtel imedhamiria kusaidia shule kwa kutoa vifaa vya mbalimbali ikiwepo vya kufundishia ili kuhakikisha elimu bora inatolewa kwa wanafunzi na jamii kwa ujumla.

"Tunatambua elimu ndiyo ufunguo wa mafanikio hivyo tunashirikiana na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kuinua kiwango cha elimu sio Mwanza tu bali Tanzania kwa ujumla.

Alisema Airtel itaendelea kusaidia shule kwa kutoa vitabu na madawati ikiwa ni sehemu ya shughuli za kusaidia jamii,nia ikiwa kuzifikia shule nyingi zaidi katika mikoa yote ya Tanzania.

Meneja wa shughuli za kijamii wa Airtel,Bi. Tunu Kavishe alisema kampuni hiyo inaelewa uhaba wa madawati na vifaa vya kufundishia hivyo aliahidi kuongeza nguvu kusaidia sekta ya elimu.

Alisema Airtel Tanzania inatoa fursa sawa kwa shule zote katika mikoa yote nchini na kuhakikisha misaada wanayotoa inawafikia wanafunzi nchini kote.

“Tunayo malengo ya dhati kusaidia kuinua kiwango cha elimu hapa nchini na kuhakikisha kinaongezeka, hasa kupitia upatikanaji wa vitabu kwa wanafunzi wa shule za sekondari"alisema Kavishe.

Alisema tangu Airtel ilipoanza mpango wa kusaidia vitabu kwa shule mbali mbali za sekondari nchini miaka saba iliyopita wameshazifikia zaidi ya shule za sekondari 800.

Bi. Kavishe alisema
Kampuni ya Airtel imekuwa mstari wa mbele kuchangia sekta ya elimu hapa nchini.

mwisho

No comments:

Post a Comment