TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Tuesday, 26 April 2011

Eleven Fighter mabingwa Kizoka Cup

Na Mwandishi Wetu

MASHINDANO ya Kizoka Cup yaliyoandaliwa na Taasisi ya Keko Mwanga Development Foundation (KEMWADEFO) ambayo Bw. Peter Mwenda ni Katibu wa Taasisi hiyo, mashindano yaliyoanza Januari 15 yamefikia kilele Jumatatu ya Pasaka kwenye viwanja vya Sigara, Dar es Salaam.

Katika fainali hizo timu ya Eleven Fighter ilitwaa ubingwa baada ya kuichapa Kona Boys kwa bao 1-0 katika fainali zilizokuwa na ushindani mkubwa ambako wageni waalikwa Rais wa TASWA, Juma Pinto na Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Kipolisi wa Temeke, David Misime walihudhuria.

Mshindi wa kwanza alizawadiwa jezi, kikombe na mipira miwili na fedha taslimu sh. 550,000, mshindi wa pili jezi na sh. 350,000 na mshindi wa tatu mipira miwili na sh. 50,000 ambako kila timu ilipewa nishani moja.

No comments:

Post a Comment