Wanafunzi sita kwenda Uturuki
Na Peter Mwenda
WANAFUNZI sita wa shule za Feza wameshinda nafasi ya kwenda nchini Uturuki kuwakilisha Tanzania katika mashindano ya kuimba kutumia lugha ya Kiswahili na Kituruki.
Akitoa zawadi kwa washindi wa fainali za mashindano ya Olympiads, Balozi wa Uturuki nchini, Dkt. Sander Gurbuz alisema amefurahishwa kuona watanzania wanaijua lugha ya Kituruki kwa ufasaha.
Balozi huyo alishauri uongozi wa Shule za Feza kuendeleza mashindano hayo kwani yanaibua vipaji vya vijana,kutangaza utamaduni wa Tanzania na kuwakutanisha na wenzao wa Uturuki.
Mkurugenzi wa Shule za Feza nchini, Ibrahim Bicakci alisema mashindano hayo ambayo yalianza mwaka 2006 wanafuynzi wengi wamewahi kwenda Uturuki kushindana.
Ibrahim alisema fainali za mashindano ya Olympiads yamempa nafasi Fauzia Bhafadhil na Irene Nderiso kushika nafasi za kwanza na kupata zawadi ya dola 150 kila mmoja.
Wengine waliopata nafasi za kwenda Uturuki ni Johannes Kihanda na Karimu Rashid walioshika nafasi ya pili na kuzawadiwa dola 100.
Nafasi ya tatuilikwenda kwa mwanafunzi Mariam Mzinge na Isabela George walioshika nafasi ya tatu na kupewa zawadi ya dola 50 za Marekani.
Ibrahim alisema mashindano ya Olympiads ambayo yatafanyika Juni mwaka huu wanafunzi kutoka shule 120 wataonesha utamaduni wa nchi zao na kuonesha uwezo wa kuimba Kituruki.
No comments:
Post a Comment