TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Monday, 17 January 2011

KEMWADEFO yapewa sh. 500,000 na Mbunge wa Temeke Mtemvu

Na Peter Mwenda

MBUNGE wa Jimbo wa Temeke, Abbas Mtemvu ametoa sh. 500,000 kwa ajili ya taasisi ya Keko Mwanga Development Foundation (KEMWADEFO) zitakazotumika kuendesha mashindano ya kumuenzi muasisi wa michezo katika Kata ya Keko, Dar es Salaam Miraji Salum 'Kizoka'.

Akizungumza katika uzinduzi wa mashindano hayo katika uwanja wa Sigara, Dar es Salaam juzi, Mbunge Mtemvu alisema michezo ndiyo njia ya pekee ya kuwafanya vijana kuepuka vishawishi na kujenga miili yao ndivyo ya kitu cha kupuuza.

Katika uzinduzi mashindano hayo ambayo yatashirikisha timu 10 za Keko Mwanga, timu ya Veterani ya KEMWADEFO ililamba mchanga baada ya kufungwa mabao 4-0 na timu ya Waandishi wa habari za Michezo (TASWA).

Mbali ya jitihada za mabeki wa KEMWADEFO, Francis Julius,Henry Nindi la Rashid Kamanyola kujitahidi kuia washambuliaji wa Twanza ilikijita inafungwa la kwanza dakika ya lilifungwa Mohamed Akida dakika ya tisa baada ya kupokea pasi ya ndefu ya Sultani Sikilo.

Bao la pili la TASWA lilifungwa na Julius Kihamba dakika ya 23 aliyeunganisha pasi ya Majuto Omari na bao la tatu lilifungwa na Khampa tena kabla ya Majuto kufunga bao la nne dakika ya 54.


Mechi ya kwanza ya ufunguzi wa mashindano hayo ilizikutanisha timu za Eleven Fighter na Bad Boys katika pambano kali lililokuwa kivutio kwa mashabiki wa soka waliohudhuria.

Pamoja ya ufundi wa kusakata soka ulioneshwa na timu mbili hizo, Eleven Fighter ilishinda  mabao 2-0 bao la kwanza likifungwa na Dini Dadi dakika ya 26 kwa mpira wa adhabu na bao la pili lilifungwa na Salum Taratibu aliyeunganisha pasi ya Januari Augustino.

mwisho

No comments:

Post a Comment