TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Friday, 14 January 2011

Askofu Pengo; Sikutarajia polisi kuua raia Tanzania

 Na Peter Mwenda

ASKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Policarp  Kadinali Pengo amesema kitendo cha askari waliopewa dhamana ya kulinda wananchi kuua watu wasio na hatia kinaashiria maafa makubwa kutokea nchini.

Akihutubia waumini wa Kanisa Katoliki wa Jimbo la Dar es Salaam katika kuadhimisha Ibada ya Misa Takatifu ya kuwaombea Wafiadini wa Pugu iliyofanyika kituo cha Hija Pugu, Askofu Pengo alisema hakutegemea jambo hilo linaweza kutokea Tanzania bara ambako kuna historia ya kuitwa kisiwa cha amani duniani.

Askofu Pengo alisema kutokana na tukio hilo amewata watanzania bila kujali madhehebu yao wasimpuuze Mungu bali warejee kumuomba ili arejeshe amani Tanzania iliyoachwa na waasisi wa nchi hii Mwalumu Julius Nyerere na Abeid Amani Karume.

Alisema wakati Tanzania inaadhimisha Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofanyika mwaka 1964, wazanzibar waliamini kwamba walikuwa wanaonewa,lazima wajitetee kwa kufanya mapinduzi wakitegemea hali bora zaidi siku za mbele.

Alisema ni jambo la kusikitisha Zanzibar kila kulipokuwa kunafanyika uchaguzi watu walikufa na kuawa lakini wananchi wa bara wakaliona kuwa hilo ni tatizo la wazanzibar.

Askofu Pengo alisema tukio la polisi kuua raia lililojitokea Arusha kwa wananchi wasio na hatia kupigwa risasi kuimetia doa Tanzania.

"Sikutegemea walinda usalama wanaweza kutumia silaha wakaua watu, wale wanaotakiwa kutetea uhai wa watanzania wanaua..."alisema Pengo.

Alisema watanzania watambue kuwa hana lengo la kueneza hisia za chuki, woga wala hisia za aina yoyote bali lengo lake kama mtumishi wa amani ni kumrudia mungu na kuomba alete amani na upendo.

Askofu Pengo alisema kitendo cha watu wakitegemea nguvu ya silaha wakifiriki kwamba njia hiyo ndiyo italeta amani huko ni kujidanyanganya na kumtukana mungu kwa vile hayo ni maandalizi ya maafa makubwa kwa ajili ya taifa la Tanzania.

Alisema watanzania wengine waungane naye kuomba laana inayonyemelea Tanzania iepukwe na hiyo imetokana kwa kumpuuza Mungu ndiyo maana tunu hiyo inapotea.

Alisema ulimwengu wa leo unaonekana kwenda kinyume na imani ya kikristo ambao inaonekana dhahiri hawana mtetezi tofauti na waislamu.

Alisema miezi ya karibuni kabla ya kuadhimisha kuzaliwa Kristu waumini wa Kikristo wameuawa katika nchi mbalimbali dunia ikiwemo Pakistani, Irani na Misri.

"Kutokana na mauaji hayo hakuna kiongozi anayejitokeza kulaani vitendo hivyo na lakini mfano Mwislamu kutotendewa haki,mmoja akisema nitachoma Kuran ulimwengu mzima unasimama kulaani"alisema Pengo.

Alisema mkristo mtetezi wake amebaki kuwa Mwenyezi Mungu pekee na amewataka wakubali kuwa tayari kuteseka kwa ajili ya imani ya dini yao.

mwisho.   
 

No comments:

Post a Comment