Na Peter Mwenda
WAZIRI wa Mambo ya Ndani,Shamsi Vuai Nahodha jana aligoma kula chakula kilichoandaliwa kwa ajili yake na msafara wake katika Kampuni ya Knight Support Tanzania Ltd baada ya mmiliki wake David Sutton kuonesha utovu wa nidhamu.
Akiwa katika ziara ya kutembelea kampuni binafsi zinazozima moto mkoa wa Dar es Salaam, Waziri Nahodha alishangaa kuona mwekezaji ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Knight Support Tanzania Ltd,Bw. David Sutton kusimama ghalfa na kutishia kuondoka katika kikao.
Kitendo hicho kilitokea wakati Waziri Nahodha akiwa anamhoji ana kwa ana na Mkurugenzi huyo aeleze sababu zinazomfanya atake alipwe sh. mil. 5 kabla ya kwenda kuzima moto na kama anajua masharti aliyopewa katika leseni yake.
Kitendo hicho kilimkasirisha Waziri Nahodha na kumwambia mwekezaji huyo ajue kuwa hayupo kwa ajili ya kuhudumia wananchi wa Tanzania mbali ya utetezi wake kuwa amewahi kuzima moto maeneo mengi bila kudai fedha.
Waziri Nahodha alionesha waziwazi kuwa kitendo hicho hakikumpendeza hivyo aligoma kula chakula kilichoandaliwa kwa ajili yake na msafara wake hata pale Mkurugenzi huyo alipoomba radhi.
"Mimi siwezi kula chakula, alisema Nahodha huku Kamishna Mkuu wa Zimamotona maofisa wengine waliofuatana naye nao kugoma kula chakula hicho.
No comments:
Post a Comment