TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Wednesday, 29 December 2010

"Kuwapa tuzo askari polisi kunaongeza motisha"

Na Peter Mwenda
WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha ameliagiza Jeshi la Polisi Tanzania kuendeleza mpango wa kuzawadia na kutunuku maofisa na askari waliotekeleza majukumu yao kwa umakini na uadilifu.

Akizungumza wakati wa gwaride la kutunuku sifa na zawadi kwa jeshi la Polisi jana, Bw. Nahodha alisema utaratibu wa kutoa zawadi utaongeza motisha, ari na moyo wa kujituma kwa waliopata zawadi hizo kuongeza tija.

"Wataalamu wa menejimenti wanasema mfanyakazi anapopewa tuzo huongeza tija na ufanisi kazini lakini mfanyakazi huyo anapofanya vibaya hapana budi pia lazima apewe adhabu ili abadili tabia" alisema Bw. Nahodha.

Alisema utaratibu huo utaleta mabadiliko makubwa katika utendaji wa jeshi la Polisi Tanzania kuahidi kutekeleza mambo yote yenye lengo la kuimarisha utendaji kazi.

Awali wakati akitunuku tuzo kwa askari polisi waliofanya vizuri katika utendaji wao kwa kukataa kupokea rushwa, kupambana na majambazi wa kutumia silaha na kazi nzuri ya kusimamia Uchaguzi Mkuu wa 2010, Bw. Nahodha alilitaka jeshi hilo kuwa wabunifu na wachapa kazi.

Pia aliwataka wananchi kuchangie na kushirikiana na jeshi la Polisi kuleta amani ambayo alisema ndiyo njia ya haraka ya kufikia maendeleo kufanana na nchi nyingine kama Dubai.

Katika hafla hiyo, iliyohudhuriwa na Inspekta Jenerali wa zamani, IGP Omari Mahita, IGP Said Mwema alisema jeshi hilo limepokea maagizo hayo ya kuahidi kuyafanyia kazi.

Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Bw. Suleiman Kova alikabidhi baiskeli 100 zilizotolewa na Kampuni ya Home Shipping Centre zenye thamani ya sh. mil.25.

Kampuni nyingine iliyotoa mchango wake kwa jeshi hilo ni Benki ya Akiba Commercial ambayo ilitoa mchango wa Sh. mil. 1 kwa ajili ya kuzawadia askari hao.

mwisho.

No comments:

Post a Comment