Na Peter Mwenda Kihansi, Mtera
MABWAWA ya kufua umeme ya Kihansi na Mtera yamejaa maji na uzalishaji umeme kurejea hali ya kawaida baada ya mvua nyingi kunyesha kutoka Desemba mwaka huu.
Katika bwawa la Kihansi ambalo mashine zake tatu huzalisha umeme wa megawati 180 za kuingia katika gridi ya taifa mashine zote tatu zimewashwa na kuzalisha umeme.
Katika kituo cha Mtera ambacho huzalisha megawati 80 kutokana na mashine mbili nako maji yamejaa na maji hayo hayo yanakwenda kuzalisha umeme mwingine wa kituo cha Kidatu na kuashiria kumalizika kwa mgawo wa umeme Tanzania.
No comments:
Post a Comment