TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Saturday, 18 December 2010

Abuu Semhando hatunaye tena duniani

Na Peter Mwenda
SIKU mbili baada ya kuzikwa mwanamuziki nguli nchini Dkt. Remmy Ongala kuzikwa, muasisi wa bendi ya African Stars (ASET) maarufu kama Twanga Pepeta, Abuu Semhando'Baba Diana' amefariki dunia baada ya pikipiki aliyokuwa akiendesha kugongwa na gari na kufa papo hapo.

Akithibitisha kifo cha Semhando, Meneja wa ASET, Martin Sospeter alisema Semhando alifariki baada ya pikipiki yake kugongwa kwa nyuma na gari aina ya Benz na kumrusha mbele na kumkanyaga juu.

"Hapa tulipo tumechanganyikiwa hata Mkurugenzi Asha Baraka si kama hataki kupokea simu bali amechanganyikiwa hatujui cha kufanya lakini msiba upo Mwananyamala Kisiwani nyumbani kwake na kesho (leo) alfajiri tunaondoka kwenda kuzika Muheza Tanga" alisema Meneja Martin.

Alisema marehemu Semhando ambaye ni muasisi wa muziki wa dansi nchini na mwanzilishi wa Twanga Pepeta na kujipatia umaarufu akiwa na bendi hiyo akishirikiana na Lwiza Mbutu, Ali Choki, Hamisi Amigolas na Ramadhani Masanja'Banza Stone' atazikwa kesho katika kijiji cha Kibanda, Muheza Mkoani Tanga.

Kifo cha Semhando kimetokea wakati mashabiki wa muziki wa dansi nchini wakiwa na majonzi ya kuondokewa na gwiji wa muziki Dkt, Remmy aliyefariki na kuzikwa katika makaburi ya Sinza kwa Remmy.

Baadhi ya wapenzi wa muziki wamepokea kwa mshtuko kifo cha Semhando wakisema pengo lake halitafutika mapema kwa sababu alikuwa kiungo kwa wanamuziki si wa bendi yake pekee bali hata nyingine za dansi, kizazi kipya, wasanii mbalimbali.

Mungu iweke roho ya marehemu mahali pema peponi, Amin.

No comments:

Post a Comment