Wakati
 Rais wa Marekani Barack Obama, akitarajia kutua kesho nchini Tanzania 
kwa ajili ya ziara ya siku mbili, Wasanii Masanja Mkandamizaji kutoka 
kundi la Ze Comedy  na msanii wa muziki wa kizazi kipya, Shilole, wao 
wametua kwenye ardhi ya Obama, kama wanavyoonekana pichani na 
 mwenyekiti wa kamati ya maandalizi wa sherehe ya miaka 3 ya Vijimambo 
na tamasha la Utamaduni wa Kiswahili, Bw. Baraka Daudi,wakati akiwapokea
 kwenye Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Dulles uliopo Sterling, 
Virginia, tayari wasanii hao kufanya makamuzi katika Tamasha hilo la 
Vijimambo.
 Asha
 Riz mjumbe aliyewawakilisha Tano Ladies kwenye mapokezi hayo akipata 
picha ya pamoja na wasanii Masanja Mkandamizaji na Shilole mara tu 
walipowasili uwanja wa ndege wa  kimataifa wa Dulles uliopo Sterling, 
Virginia.
 Asha Riz katika picha ya pamoja na Shilole.
Wasanii Masanja Mkandamizaji na Shilole wakielekea kuchukua usafiri kuelekea Washington, DC kwa Obama
 Shilole katika ukodak moment alipokua uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dulles uliopo Sterling, Virginia.
 Masanja Mkandamizaji kwenye Ukondak Moment uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dulles uliopo Sterling, Virginia.
 Masanja na Shilole katika picha ya pamoja.
 Msanja akionyesha uwanja wa Julius Nyerere wa Marekani " NIMETUA KWA OBAMA UNABISHA???"
No comments:
Post a Comment