Na Peter Mwenda

MBUNGE wa Temeke, Bw. Abbas Mtemvu amesema benki za kigeni hazijawahi kuwasaidia wajasiriamali wa Tanzania kutokana na riba kubwa zinazotozwa baada ya kutolewa mikopo.

Akizungumza katika uzinduzi wa kikundi cha VICOBA cha Safina cha Keko juzi, Bw. Mtemvu alisema riba zinazotozwa na mabenki ya nje inawanufaisha wenyewe lakini wajasilimali wa Tanzania ambao wanahaha kutafuta mitaji wanashindwa kupata mikopo ya riba ndogo.

"Mabenki yote hayana msaada, yamekuja kuchuma tu na siyo kusaidia watanzania, serikali inatuambie tuanzishe VICOBA lakini mitaji tutapata wapi?alisema Bw. Mtemvu.

Alisema mikopo iliyotolewa na Rais Jakaya Kikwete maarufu kama mabesa ya JK yamekqwenda kwa vigogo wachache na kuwaacha wananchi wa kawaida wenye nia ya kujikwamua kimaisha kwa kuanzisha miradi bila kujua zilikwenda.

Bw. Mtenmvu alisema benki ambazo zilianzishwa kwa ajili ya wananchi nazo zimebadilisha mwelekeo badala yake uzinawakopesha matajiri hivyo kuwaacha wananchi wa kawaida wakikwama kutokana na kukosa mitaji ya biashara.

Mbunge huyo mbaye pia ni Mwenyekiti wa wabunge wa mkoa wa Dar es Salaam alisema katika VICOBA nako kumezuika tabia ya baadhi ya viongozi kukaa na fedha za wanachama wao bila kupeleka benki.

Alisema atatumia nafasi hiyo kuwachukulia hatua viongozi wa VICOBA ambao hawajafungua akanti benki kwa ajili ya kuweka fedha za wanachama.

Mwenyekiti wa kikundi cha Vicoba cha Safina,Bw. David Nyambe alisema mikakati yao ya awali na kununua gari la wagonjwa na kuanzisha kikundi cha kuzoa taka katika eneo la Keko.

Alisema kikundi hicho kimenunua hekari 50 wilayani Rufiji na kina mtaji wa sh. mil. 29 kwa ajili ya kukopesha wanakikundi ambao hautoshi kukopa mara tatu zaidi.

Naye mratibu wa asasi ya UYACODE, Bw. Aldo Mfinde alisema ili kupunguza umaskini nchini ni pale ambapo wananchi wataamua kujiunga kuanzisha vikundi vya VICOBA

mwisho