TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Tuesday 27 September 2011

CUF yatangaza CCM kutoa rushwa chakula, sukari Igunga
.Yaionya CHADEMA isiifuatilie kwenye mikutano yake
.CCM yaruka, gari la Rage laparamia mkutano wa CUF
.CUF sasa kufanya kampeni kwa helkopta

 Na Peter Mwenda, Igunga

CHAMA cha Wananchi (CUF) kimeituhumu Serikali kuwa inataka kugawa chakula cha msaada na sukari kwa wananchi siku mbili kabla ya kupiga kura katika uchaguzi mdogo wa mbunge wa Jimbo la Igunga kama rushwa ili wakipigie kura CCM.

Naibu Katibu Mkuu wa CUF Bara, Bw. Julius Mtatiro akizungumza na waandishi wa habari jana alisema serikali ya CCM imepakia shehena ya sukari kwenye malori saba na chakula cha msaada kwa ajilli ya kugawa katika kila kaya jimbo la Igunga Septemba 30 na Oktoba Mosi ikiwa siku moja kabla ya kupiga kura.

“Waache wananchi wapige kura baadaye waendelee kugawa chakula cha msaada, CUF tumejipanga vya kutosha kuzuia,tutayakama magari hayo na kutawaita waandishi wa habari  hawatagawa mahindi katika jimbo hili Septemba 30 na Oktoba Mosi, hili tutalidhibiti kwa sababu tyumisha lijua hatuwezi kukubali haki za watanzania kuchagua kiongozi bora kwa ajili ya kilo moja ya sukari , “alisema Bw. Mtatiro.

Alisema kama wananchi wamekaa na njaa kwa muda wote bila kufa hawawezsi kufa kwa siku moja ambayo kunafanyika uchaguzi kwa sababu hiyo ni rushwa ya waziwazi na kuitaka Tume ya Uchaguzi kushughulkikia suala hilo kwa kuzuia.

Pia Bw. Mtatiro alisema vijana wa CCM wamemaliza mafunzo yao katika kambi Shinyanga “Janjawidi’ ili kutengeneza vitisho kwa wananchi hasa katika yale maeneo ambayo hawaungwi mkono katika kata 19 kati ya 26 za Jimbo la Igunga ili watu waachwe na majereha baada ya uchaguzi.

Alikitaka  CCM ikubali kuliachia Jimbo la Igunga kwa sababu wamebanwa katika kila kona kwani  wanayo majimbo  lukuki katika nchi nzima ambayo yanawatosha na kuiomba Jeshi la Polisi kuchukua hatua za kuwathibiti  kabla ya kuleta madhara.

Alisema CUF itachukua majina yote ya wapiga kura na kuingiza kwenye komputa ili kukabiliana na ujanja wa CCM kuondoa majina hayo siku ya kupiga kura na kubandika mengine ili kuwanyima nafasi wale wenye mwelekeo kwa upinzani.

Bw. Mtatiro alisema Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini Bw. John Tendwa aache kuingilia  uchaguzi wa Igunga pale aliposema uchaguzi huo usimamishwe kwani anatakiwa awaachie Tume ya Uchaguzi (NEC).

Pia alikitaka CHADEMA kiaache kukifuata chama hicho katika mikutano yake ya kampeni kwani kufanya hivyo ni kutibua mbinu za ushindi ilizojipangia katika uchaguzi wa Igunga.
“Tunaomba wenzetu wa Chadema waache kutufuata fuata katika mikutano yetu, mimi mwenyewe nimekutana nao mara nne, hakuna haja ya kuanza kufuatiliana wasifuate siasa za CCM wanatuma usalama wa taifa kutufuatilia wakiacha kuzuia twiga na nyara za Serikali zikisafirishwa” alisema Bw. Mtatiro.

Alisema tunahitaji baada ya uchaguzi wananchi wa Igunga waishi kwa amani na utulivu wasiachwe wamekufa au kujeruhiwa wakati bado shida zao za maji, afya, elimu na maisha bora yakiwa kitendawili.

Bw. Mtatiro alisema katika maandalizi ya mwisho ya CUF imeongeza nguvu kwa wabunge wengine 13 kuwasili katika Jimbo la Igunga kummwombea kura mgombea wao Bw. Leopold Mahona.

Alisema kwa mara ya kwanza CUF itatumia helkopta katika siku nne zilizobaki ili kurahisisha mgombea wao kuwafikia wananchi kwa urahisi baada ya kuona gharama zake ni za kawaida ambako wanatarajia kufanya mikutano 16 kwa siku katika vijiji 96 vya Jimbo la Igunga.

Akijibu tuhuma hizo Katibu wa Fedha na Uchumi wa CCM ambaye pia ni Meneja wa Uchaguzi wa Igunga, Bw. Mwigulu Nchemba alisema hakuna mpango wala mzigo wa sukari unaopelekwa Igunga kwa ajili ya kugawa.

Alisema si kweli CCM kuandaa vijana (Janjawidi) kwa ajili ya kufanya fujo na kama wamewaona hao ni vijana wa chama na kuhusu chakula hiyo ilianza kugawa kabla ya kampeni kuanza na tarehe hizo chakula kitagaiwa kama ilivyo sehemu nyingine za Iramba na kwingineko kwa uhaba wa chakula.

Wakati huo huo katika tukio jingine mbunge wa Mkanyageni Pemba, Bw. Mohamed Habib Mnyaa na Mbunge wa Viti Maalum Dodoma wamenusurika kugongwa na gari aina ya Noah liliacha njia na kuparamia mkutano wa kampeni wa CUF katika Kata ya Ziba nje ya mjini wa Igunga.

Katika tukio hilo gari la Redio ya Tabora ( VOT) T 836 AZP ambayo inamilikiwa na Mbunge wa Tabora Mjini Bw. Ismail Aden Rage ambaye hupo mjini hapa likiwa na dereva na mtu mwingine lililokuwa katika msafara wa Katibu Mkuu wa zamani wa CCM, Bw. Phillip Mangula likiwa katika mwendo kasi liliacha njia na kuangia kwenye umati wananchi waliotimua mbio ndipo polisi waliokuwepo katika mkutano huo kuwaweka nchini ya ulinzi na kuondoka nao kwenda kituo cha polisi, Igunga.

Bw. Mnyaa akizungumza baada ya tukio hilo alisema limemshtua lakini hiyo ni ajali kama nyingine hivyo alisema huenda dereva alikuwa amelewa au alishindwa kulimudu gari hilo huku Mbunge wa Viti Maalum CUF Dodoma Bibi Moza Said akisema tukio hilo limemshtua sana na kumfanya BP ipande.

mwisho

No comments:

Post a Comment