Na Peter Mwenda
WAGOMBEA wawili wa Udiwani wa Kata za Kivule na Kitunda katika Jimbo la Ukonga wamekemea vikali uvumi ulioenea kutoka kwa wakazi wa maeneo hayo kutishia kutompigia kura mgombea wa ubunge CCM, Bi. Eugene Mwaiposa kwa madai kuwa mila za kabila hilo zinawakataza.
Uvumi huo umekuwa ukisemwa waziwazi kuwa Wakurya ambao ni wengi katika kata za Msongola,Kivule,Kitunda kuwa ni aibu kwa kabila la Wakurya kuona mwanamke akisimama mbele yao na kutoa maelekezo ya kufanya.
Bw. Nyansika Getama wa Kata ya Kivule, Mwalimu Daniel Ryoba na Mwenyekiti wa mtaa wa Kivule Bw. Joseph Gassaya ambao ni wakurya wamesema mila hizo zimepitwa na wakati na kuwaambia waache hiyo kwa sababu ni aibu.
No comments:
Post a Comment