Mgombea Ubunge (CCM) Korogwe Vijijini Profesa Maji Marefu na Peter Mwenda walipokutana leo (Ijumaa) Dar es Salaam.
"Amini usiamini jamii ya watanzania sasa hivi HAWADANGANYIKI katika uchaguzi huu 2010. Wanajua kiongozi anaowafaa ni yule aliyekaribu nao, kati ya wananchi hao ni wale wa Korogwe vijijini waliamua kumpa tano Mganga wa tiba za Asili Tanzania Bw. Steven Hilary Ngonyani maarufu 'Profesa Maji Marefu' aliyeibuka kwa kura nyingi za ndiyo katika kura za maoni kupitia CCM".
Maji Marefu anayefanya kazi zake nchini Kenya, ni rafiki wa jamii katika kila rika wakiwemo waandishi wa habari kwani aliwahi kusafirisha waandishi 20 kwenda Kenya 'nikiwemo kama Mkuu wa msafara' kushuhudia pambano la soka kati ya timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars ' na Harambee Stars mwaka 2004 ambako tulifungwa mabao 3-0.
No comments:
Post a Comment