TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Wednesday 7 November 2018

RAMADHANI SHAURI NA AZIZI ULIZA WASAINI KUZIPIGA DESEMBA 31




Mratibu wa mpambano wa masumbwi nchini Chaurembo Parasa Katikati akiwainuwa mikono juu mabondia Azizi Uliza kushoto na Ramadhani Shauri baada ya kusaini mkataba wa kuzipiga Desemba 31 katika uwanja wa Kinesi uliopo Shekirango Picha na Super D Boxing News

Mabondia Azizi Uliza kushoto wakitazamana kwa usongo mara baada ya kusaini mkataba wa kuzipiga Desemba 31 katika uwanja wa Kinese Shekilango

Mratibu wa mpambano wa masumbwi nchini Chaurembo Parasa Katikati akiwa na mabondia Ramadhani Shauri kushoto na  Azizi Ulizabaada ya kusaini mkataba wa kuzipiga Desemba 31 katika uwanja wa Kinesi uliopo Shekirango Picha na Super D Boxing News


Na Mwandishi Wetu

MABONDIA Ramadhani Shauri na Azizi Uliza wame saini mkataba wa kuzipiga Desemba 31 katika uwanja wa Kinesi Dar es salaam uliopo maeneo ya Shekilango

akizungumza mratibu wa mpambano uho Chaurembo Palasa amesema kuwa wamejizatiti kuinuwa mabondi yeye na kampuni ya Ijuka Sports ambao wanajishughulisha na kuinuwa mchezo wa masumbwi nchini

aliongeza kwa kusema kuwa mabondia wengi wana ndoto ya kufika Marekani kucheza mchezo wa ngumi sasa kampuni hii imeanza na mapambano haya ili mradi mabondia wapate nafasi ya kupigana Marekani ambapo mchezo huu unakubalika kwa asilimia mia moja bila kupingwa mabondia watakaofanya vizuri watakwenda kupigana U.S.A

aliendelea kwa kusema siku hiyo mbali na mpambano uho kutakuwa na mapambano mengine ya kukata na shoka wakati Hussein Itaba atazipiga na Kanda Kabongo na Tonny Rashidi atazipiga na Nassoro Madimba kutoka Bagamoyo maeneo ya Kiwangwa na Rolen Japhert atazikunja na Mohamedi Kashinde 'Simba wa Mbagala' nae Baina Mazola ataoneshana umwamba na Faraji Sayuni

siku hiyo pia kutakuwa zikiuzwa DVD mpya za masumbwi ambazo zinaonesha mafunzo mbalimbali ya mchezo wa ngumi yanavyoanza hatua kwa hatua

mpaka kujua kitu kamili katika

mchezo huo pia kunakuwa na mapambano ya mabondia mabigwa wa dunia wa mchezo huo kama Floyd


Maywether, Manny Paquaio,mike Tyson, Mohamed Alli pamoja na mabambano ya ngumi ya ndani zilizo taharishwa na kocha maili wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' ambaye anajishughulisha na uzaji wa vifaa mbalimbali vya ngumi nchini kama vile Glove gumshirt clip bandeji bukta protecter na vifaa vingine

No comments:

Post a Comment