TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Monday, 13 February 2017

Tamasha la wasanii SHIWATA kufanyika Mkuranga Julai

 Na Peter Mwenda
  

MTANDAO wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) umeandaa Tamasha la Michezo na Sanaa katika kijiji cha Wasanii Mwanzega,Mkuranga Julai mwaka huu ambapo wanamichezo na wasanii zaidi ya too watashiriki.
  

Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Taalib alisema michezo na burudani ambayo itafanyika ni pamoja na soka, mpira wa kikapu, wavu, riadha,ngumi mashindano ya magari, pikipiki, baiskeli na mpira wa pete.
  

Michezo mingine ni mchezo wa kujilinda wa Tae kwon-do, Wu- Shu, Sarakasi, ngoma, maigizo ya filamu, tamthilia, kwaya kienjili, Kaswida, muziki wa asili, muziki wa dansi,muziki wa kizazi kipya na ushairi.
 

Mwenyekiti Taalib alisema hiyo ni fursa nzuri kwa wasanii na wnamichezo hapa nchini kwani inatarajiwa kufanyika hapa nchini kila mwaka na milango iko wazi kwa wasanii na wanamichezo mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi watapata nafasi ya kukutana katika kijiji chao kwa pamoja na kubasilishana mawazo na utaalamu kwa malengo ya kukuza na K uendeleza vipaji vyao pamoja na kudumisha umoja na mshikamano Kati ya wanamichezo na wasanii hapa nchini.  

Tamasha hili ambako awali lilikuwa kufanyika Juni mwaka huu limesogezwa mbele hadi Julai 13,2017 ili kupisha wasanii na wanamichezo kwa ajili ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na sikukuu ya Eid al fitri.
  

SHIWATA katika Tamasha hilo itatoa chakula kwa wasanii na wanamichezo watakaoshiriki Tamasha hilo isipokuwa washiriki wtajitegemea wenyewe gharama as usafiri wa kwenda na kurudi.
  

Mwenyekiti Taalib alisema milango iko wazi kwa nafasi as USHIRIKI kwa klabu as michezo mbalimbali na makundi is wasanii kushiriki katika Tamasha hilo.
  

Orodha ya majina ya klabu na vikundi,bendi na washiriki na watu binafsi wajulishe ofisini SHIWATA kwa uratibu wa michezo hiyo kabla ya 28/2/2017 Indonesia majina ya timu pamoja na viongozi na namba ask za simu na michezo wanayoomba kushiriki.
 

Kutakuwa na mkutano wa viongozi wote watakaoshiriki Tamasha hilo 11/3/2017 saa 4 ukumbi wa hotel I ya Cyrstal Palace,Ilala Bungoni ili kupata taarifa za Tamasha hilo.
  

KATIKA mkutano huo pia zitatolewa taarifa ya jinsi wasanii na wanamichezo wanavyoweza kujiunga na SHIWATA na kupata fursa ya kujenga nyumba zao binafsi katika kijiji cha wasanii.
  

Mwisho

No comments:

Post a Comment