TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Monday 1 February 2016

Chelsea,Man City kuchuana FA

Chelsea watacheza nyumbani dhidi ya Manchester City katika raundi ya tano ya Kombe la FA,Klabu ya League One Shrewsbury Town, iliyoorodheshwa ya chini zaidi miongoni mwa timu zilizosalia kwenye shindano hilo nayo itakuwa mwenyeji wa Manchester United katika uwanja wa New Meadow.

Mabingwa watetezi Arsenal watakutana na Hull, marudio ya fainali ya 2014. Hii itakuwa mara ya tatu mfululizo kwa klabu hizo mbili kukutana katika dimba hilo. Gunners waliwabandua Hull kwenye raundi ya tatu mwaka jana baada ya kuwashinda 2-0,Crystal Palace nao wakitembelea Tottenham na Bournemouth wacheze nyumbani dhidi ya Everton kwenye michezo itakayoshirikisha klabu za Ligi ya Premia pekee.

No comments:

Post a Comment