TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Friday 17 July 2015

Shabiki Yanga achukua fomu ya Udiwani Tabata

Na Mwandishi Wetu

SHABIKI wa Klabu ya Yanga, Sudi Kassim Sudi maarufu kwa jina la Big Respect amechukua fomu za kugombea udiwani wa Kata ya Tabata.

Sudi aliyesindikizwa na familia yake kuchukua fomu hizo aliahidi kuwainua vijana katika michezo kuongeza ajira kwani anaamini katika kata hiyo wapo wachezaji wengi wenye vipaji na uwezo wa kucheza mpira Tanzania na nje ya nchi kama wataendelezwa.
Alisema amekuwa shabiki na mpenzi wa michezo nchini na katika kata hiyo kwa muda mrefu hivyo alipoamua kuchukua fomu akipata nafasi hiyo atakuwa kiongozi wa jamii hasa  vijana wa Kata hiyo kwenye michezo kwa kugawa vifaa vya michezo na kuwakwamua kimaisha.
Alisema sababu nyingine iliyochangia kuchukua fomu za udiwani ni kutaka kushirikiana na wakazi wa eneo hilo kuondoa kero zinazoendelea kuwatesaza miundombinu na maji safi na bora.

Alisema baada ya CCM kumteua Dkt. John Magufuli kuwa mgombea urais ni moja ya sababu iliyochangia kuwa na ari ya kuchukuafomu kwani ana imani naye kuwa ni mchapakazi.
Awali Katibu wa CCM kata ya Tabata, Ibrahim Mjanakheri aliyekabidhi fomu hizo alisema kutoka CCM imteue Dkt. Magufuli kuwa mgombea wao wa Urais hata wapinzani wameshikwa na kigugumizi cha kuwasimamisha wagombea mwaka huu.
Alisema Dkt. Magufuli ameongeza ari kwa wanaccm wanaochukua fomu wakiamini kuwa chama hicho kimerjipanga kuhakikisha kinapata ushindi wa kishindo.
mwisho

No comments:

Post a Comment