Na Mwandishi Wetu
MCHEZAJI wa zamani wa Timu ya Taifa
ya Tanzania (Taifa Stars), Simba, Kajumulo na Mirambo ya Tabora, Kureshy
Ufunguo ameamua kurudi uwanjani safari hii kuanzia Soka ya Watoto
(Academy) ili kusaka vipaji vya wachezaji wa kuunda Stars baadaye.
Akizungumza
Dar es Salaam jana, Kureshy ambaye aliwahi kuchezea Stars kwa nyakati
tofauti alisema anasikia uchungu kuona timu ya Taifa inafanya vibaya mara
kwa mara wakati kuna watoto wengi wenye vipaji ambavyo vikiliendelezwa
vitaibua wachezaji wazuri.
Alisema amefanya mazungumzo na
baadhiu ya maduka ya kuuza vifaa vya michezo likiwemo Isere Sports na
kuchagua vifaa ambavyo ataanzia katika kufundisha watoto hao.
Kureshy
alisema kwa kuanzia atakuwa anawakusanya watoto katika Klabu
aliyoianzisha Kitunda, Kivule ambapo ataanza kuwafundisha kwa nadharia
yaani darasani na baadaye uwanjani ambako atatumia uwanja wa Shule ya
Sekondari, Misitu, Kivule Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa
Masoko wa Isere Sports, Abbas Ally alisema Kampuni yake itasaidia kutoa
vifaa vya kuanzia mazoezi kama vikinga ugoko (shin guard), mipira na
jezi za mazoezi.
Alisema Kampuni itaendelea kutoa
misaada kwa mchezaji huyo kwani ni wachache wenye ndoto ya kufufua soka
ya Tanzania ambayo kwa sasa Stars haifanyi vizuri katika mashindano
mbalimbali ya kimataifa.
Mwisho
No comments:
Post a Comment